Mdau namba moja wa blog, KC akiwa amepozi na bonge la T-shirt lenye maneno ya kijanja "Kwenye msafara wa mamba nami nimo". KC pia ndiye mtaalamu wa kuprint t-shirt hizo ambaye anapatikana kunako ofisi yake iliyopo pande za Mwenge, Dar es salaam. kama na wewe utapenda kung'aa na pamba hizi cheki nami 0715 110 173.
About Me
MC Logo
PHOTOS
SHOW BIZ HITZ
BONGO HITZ
OLD SCHOOL FLAVA
Blog Archive
-
▼
2009
(77)
-
▼
September
(19)
- MDAU NA BONGE LA T-SHIRT
- KAMATA T-SHIRT ZA KIJANJA
- MKUBWA FELLA, AFANDE ULINGONI!
- SCOUT O, K-MAN NA NGOMA MPYA
- DJ CHOKA ALA SHAVU ZIZZOU ENTERTAINMENT
- A.Y NDANI YA MALAYSIA
- D'BANJ KUDONDOKA BONGO
- TMK WALIVYOPOTEZA COCO BEACH EID PILI
- FUTURU YA MWISHO KABLA YA EID
- CHIGUNDA ANASUBIRI WAIFU
- KAMATA NDINGA MWANANGU
- KAZI NA DAWA JAMANI
- WAPE SHAVU A.Y, SHAA TUZO ZA MTV
- KIFO CHA MPAKANJIA BADO NI SIMANZI
- QUEEN DOREEN BACK AGAIN
- KIBOOT NA SALAAM KUTOKA SAUZI
- MKUBWA FELLA NA NGOMA MPYA
- APEX RECORDS YAANZA NA MCHAJI
- CHEKI MAISHA YA RAIS WA MANZESE
-
▼
September
(19)
G5 WORLD
ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU
Kama wewe ni Mbongo halisi unatakiwa uoneshe uzalendo kwa kugonga bidhaa za home, ule wakati wa kuvaa nguo zenye maandishi ya kufagilia vitu vya nje umepitwa na wakati. Hivi sasa wajanja wanathamini vitu vya nyumbani. T-Shirt hizi zinapatikana pande za Sinza, Bamaga kwa bei ya jumla na reja reja, pia tunapokea oda kutoka sehemu mbalimbali nchini. Unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0715-110 173. email:mcgeorge2008@gmail.com.
Ishu iko hivi, ebwanadaah ilipiga stori na mastaa hao kwa nyakati tofauti ambapo wa kwanza alikuwa Sele aliyesema kuwa Mkubwa amekuwa akimfanyia kitu kibaya kwa kutaka kumpoteza kwenye game.
"Fella hanipendi, nikifanya shoo na Wanaume mara nyingi ananizimia MIC au anakorofisha mitambo ili sauti yangu isisikike vizuri. Fella hanipendi na mimi najua hilo," alisema Sele.
Akijibu hoja, Mkubwa alisema kuwa anasikitishwa na kauli za Afande na kwamba hakuna ukweli katika hilo na kuongeza kwamba ingekuwa vema mfalme huyo anayetokea pande za Moro akataja shoo ambazo alimzimia vyombo.
"Mimi naangalia mafanikio na maendeleo ya wasanii wa kundi langu, si kuendekeza roho mbaya kwa wengine," alisema Mkubwa.
Bifu ni hilo, nani mkorofi? Kama una data zimwage kupitia namba 0715-110 173 au mcgeorge2008@gmail.com. Read More......
Mbali na yeye, mshikaji wa karibu, K-Man naye pia ameachia kazi yenye jina la Wamesahau chini ya prodyuza Lamar. Kazi kwenu wadau wa burudani, madogo wamekuja kivingine sana. Read More......
Aliyekuwa dj wa Prof. Jay Hugoline Mtambachuo Martin a.k.a Dj Choka amekula shavu la ukweli ndani ya kampuni ya Zizzou Entertainment kama dj wa wasanii waliopo chini ya lebo hiyo.
Nawazungumzia Ngwea, Blue, Squeezer, Steve, Bushoke na wengine kibao.
"Najisikia faraja sana kwasababu nimeyaanza maisha yangu upya kabisa toka nilivyoondoka kwa Bro Jay, pia najishughulisha kusambaza habari za wasanii wote wa bongo katika blog yangu inayoitwa www.djchoka.blogspot.com", alisema Choka.
Msanii Ambwene Yesaya A.Y ambaye alikwea pipa mwishoni mwa wiki iliyopita kuelekea Malaysia tayari ameshadondoka pande hizo na jana Alhamisi aligonga shoo ya funiko kunako Jiji la Kuala Lumpur.
Akipiga stori na ebwana daah kwa njia ya simu kutoka pande hizo jamaa alisema kwamba kila kitu kuhusu ziara yake hiyo kimekwenda fresh na kwamba anatarajia kurudi Bongo Jumapili ya wiki hii kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wa kuwania tuzo za MTV Afrika kama Msanii Bora wa Hip Hop akichuana na mastaa kama Jay-Z na Kanye West.
Ili kumuwezesha kuibuka na ushindi A.Y andika neno BHH AY kisha tuma kwenda namba 0789 777 333. Ili kumuwezesha Shaa ambaye anawania tuzo ya Msanii Bora Anayechipukia andika neno BNA SHAA kisha tuma kwenda namba 0789 777 333 Read More......
Katika kusheheresha tuzo za MTV Afika zinazotarajiwa kutolewa mwezi ujao pande za Kenya, mchizi anayefanya vyema na ngoma kadhaa hivi sasa, Dapo Daniel Oyebanjo a.k.a DÕBanj kutoka Nigeria anatarajiwa kudondoka Bongo hivi karibuni kama mgeni mwalikwa kunako shoo yenye jina la Road to MTV Africa Music Awards (MAMA) itakayopigwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas Oktoba 3, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mratibu wa ishu hiyo, Christina Mosha 'Seven' shoo hiyo ambayo hufanyika kila mwaka na sehemu tofauti yakiwa ni maandalizi ya kuelekea kunako tuzo hizo safari hii itafanyika Bongo ambapo mbali na mkali huyo kutoka Nigeria pia wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania 'awadi' hizo Ambwene Yesaya 'A.Y' na Sara Kaisi 'Shaa' wataangusha burudani ya ukweli.
"Pia msanii kama Profesa Jay ambaye atakuwa ni mgeni mwalikwa katika tuzo hizo tutakuwa naye katika shoo hiyo ya Bilicanas ambayo itaanza saa tatu usiku na kuendelea kwa kiingilio cha shilingi 15, 000 kila mtu. Kwa ishu zaidi watu wanaweza kutembelea website yetu ambayo ni www.mama.mtvbase.com," alisema Seven.
Pia mratibu huyo amewaomba Watanzania na wapenzi wa burudani kwa ujumla wanaombwa kuendelea kuwapigia kura A.Y na Shaa ili waweze kuleta heshima Bongo kwa kuibuka na tuzo hizo. 'Kumpigia kura A.Y andika neno BHH AY kisha unatuma kwenda namba 0789 777 333. Ili kumuwezesha Shaa ambaye anawania tuzo ya Msanii Bora Anayechipukia andika neno BNA SHAA kisha tuma kwenda namba 0789 777 333.
Msanii huyo (katika picha kubwa) alisema kwamba programu hiyo yenye jina la 'Shinda kuwa mke wa Chegge' imemkutanisha na wasichana wengi lakini anaamini atampata mmoja ambaye ni mwema. Kupitia programu hiyo msichana ambaye atashinda kuwa mke wa Chegge atatajwa wiki ijayo.
Hivi sasa Chegge amesimama na ngoma mbili, hewani, Karibu Kiumeni aliyomshirikisha Ngwea na Running Low remix aliyogonga na Wahuu wa Kenya, siku kadhaa zijazo ataachia kali nyingine, aliyompa shavu Lady Jaydee, unajua ni ipi? Kaa tayari
A.Y anachuana na wakali kama Jigga katika tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop, Shaa anaparurana na wasanii wa mataifa mengine katika tuzo ya Msanii Bora Anayekuja.
Wanaweza kushinda ikiwa tu hautobana kuwapigia kura, kumchagua AY andika neno BHH AY kwenda namba 0789 777 333 na Shaa unaandika BNA SHAA kwenda namba 0789 777 333. Unaweza kupiga kura mara nyingi kadiri uwezavyo ili kuipa heshima Tanzania katika eneo la muziki.
Mpakanjia na Amina enzi za uhai wao. Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi
Kupitia safu ya 'Mwana mpotevu' inayopatikana pia ndani ya gazeti la Ijumaa ShowBiz tutakuwa tukiwatafuta mastaa wa kitambo ambao waliwahi kufanya vyema kupitia sanaa zao kisha wakapotea. Kubwa zaidi litakuwa ni kwanini wapo kimya na huko waliko kwa wakati huo wanapiga ishu gani.
Kwa kuanza leo tunadondoka na binti aliyeingia kwenye game ya muziki wa kizazi kipya akiwa na umri mdogo na kufanya kazi kadhaa kisha kupotea, namzunguzia Doreen Mkude a.k.a Queen Doreen.
Alikuja kwa kasi na kushaini katika anga ya Bongo Flava kwa michano lakini ghafla ikawa jiiiii! Alipokutana na ShowBiz katikati ya wiki hii kabla ya yote alitamka kwamba sasa anarudi kamili kuwashika fans wote wa muziki.
Queen Doreen ambaye alikuwa memba active wa Kundi la Dar Scandal lililokuwa likiongozwa na Godfrey Tumaini 'Dudubaya', ameweka kweupe some issues zilizomfanya awe out of game kwa muda.
Mdada huyo alisema kuwa sababu namba moja iliyomfanya awe nje ya game ni masomo na kueleza kwamba aliona muziki Bongo si uwanja sahihi wa kuutegemea kufanya maisha ndiyo maana aliichenga Bongo Flava na kutimkia skonga.
Hata hivyo, Queen Doreen alisema kuwa kitu kingine kilichomkimbiza ni rushwa ya ngono kwa maelezo kuwa wadau wengi walikuwa wanabana kumsaidia mpaka pale atakaporidhia kuchekiwa on bed.
Mbali na hilo, aliimegea kona hii exclusive kwamba yupo anajiandaa na ujio mpya kwamba albamu yake ipo njia moja. Ni hayo tu kuhusu Doreen kwa leo. Cheki na sisi next week.
Mchizi anayewakilisha vyema Bongo Flava pande za Afrika Kusini a.k.a Sauzi, Kiboot amedondoka Bongo na salamu kibao kutoka Bondeni. Mbali na kuwa na albamu mbili mkononi, yenye ngoma za kiswahili na ya kiingereza pia anazo idea kibao za kushea na wana Bongo Flava ambazo zitawawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia ajira yao ya muziki. Mengi kuhusu mchizi usikose kucheki ndani ya Gazeti la Ijumaa kupitia safu namba moja ya burudani nchini, ShowBiz.
Bosi wa crew ya TMK Wanaume Family, Said Fella 'Mkubwa' anazidisha harakati zake kwenye muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Flava na hivi juzi ame-release ngoma mpya yenye jina la 'Tunapambana'.
Fella alichonga na kona hii kisha kuijuza ya kwamba dude hilo ambalo limewashirikisha wanawe, TMK Family ni moja ya songs zilizomo ndani ya albamu yake ambayo inapaa kitaani hivi sasa kwa jina la Mkubwa na Wanawe.
Mkubwa ambaye ali-exist katika game long time ago kama meneja wa wasanii, hivi sasa ameongeza mwendokasi kiaina kwa ku-manage artists na kushika MIC kwa wakati mmoja ambapo traki yake ya kwanza inavuta pumzi kwa jina la 2008-2009.
Studio mpya na ya ukweli iliyopo pande za Mburahati, Dar es Salaam, Apex Records imeanza kushika kasi, hivi sasa tayari imemsimamisha 'dogo' aliyekuwa anapiga kazi ndani ya kundi la 'Wachaji Zote', Heri Wilbad a.k.a Mtoto wa Binti Makombora ambaye hivi sasa anasikika na ngoma yenye jina la 'Niambie nijue' iliyogongwa na prodyuza Villy studioni hapo.
"Unajua baada ya kutengana na mshikaji kila mtu aliamua kusafa kivyake, hatimaye mimi nikashitukia nimeibukia Apex ambapo nipo lebo na tayari nimeshafanya ngoma hiyo na nyingine zinakuja chini ya prodyuza Villy ambazo kiukweli zitaniweka juu", alisema Mchaji.
Mbali na Mchaji, wasanii kibao wa muziki wa kizazi kipya wakiwemo TMK Wanaume Family wameshaanza kuibuka pande hizo na kufanya kazi kadhaa.
"Nilifurahi sana siku ya kwanza kuitwa baba"
Baada ya kucheki bonge la ‘intavyuu’ kuhusu maisha ya mwanamuziki kutoka kiumeni Chegge, wiki iliyopita, Mpaka Home bado inaendelea kusonga mbele kiubishi na kufanikiwa kuyabamba maisha mapya ya mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Hamad Ali 'Madee' a.k.a Rais wa Mazese ambaye ni memba namba wani wa familia ya Tip Top Connection.
Hapo awali tuliwahi kumtoa mchizi huyu ambaye alikuwa bado akipiga ‘life’ flani nyumbani kwao, hivyo baada ya kuhamia kwake akiwa na umri wa miaka 28 sasa, Mpaka Home imetimba kwenye makazi yake mapya, Kimara- Rombo ili kujua mengi zaidi kuhusu laifu yake cheki na intavyuu hapo chini.
Mpaka Home: Mambo Madee?
Madee: Mambo mzuka tu, karibu sana maskani.
Mpaka Home: Nashukuru sana, ila ningependa kujua unaishi na nani hapa?
Madee: Hapa nipo na washikaji zangu wananipa kampani.
Mpaka Home: Mimi nilidhani kwa kuwa umehamia makazi mapya utaniambia uko na wifi yangu?
Madee: Hapana, bado nipo nipo kwanza.
Mpaka Home: Lakini si ulikuwa na demu Madee?
Madee: Ah! Yule si alinizingua mambo flani hivi.
Mpaka Home: Sasa inakuaje katika upande wa kupika, ukizingatia huu ni mwezi wa futari?
Madee: Mimi hapa nasubiria ikifika midamida tu nachukua tambi zangu naingia zangu jikoni.
Mpaka Home: Ni tofauti gani unaiona ulipokuwa nyumbani na sasa upo kwako?
Madee: Tofauti kubwa sana, kwa maana unapokuwa nyumbani huwezi kufikiria kufanya maendeleo yako, lakini ukiwa kwako kama hivi, unajituma hata kununua sofa.
Mpaka Home: Ni kitu gani unapenda kufanya unapokuwa nyumbani?
Madee: Napenda kufanya kazi zangu kwenye Kompyuta na kupiga gitaa langu.
Mpaka Home: Wanaume wengi hawapendi kujifulia, hususani mastaa, vipi kwa upande wako?
Madee: Mimi nafanya kila kitu mwenyewe, wala hilo halinisumbui kichwa sista.
Mpaka Home: Ni msosi gani unapenda kujipikia Madee?
Madee: Napenda sana kupika wali, haunisumbui kwa sababu natumia Rice Cooker.
Mpaka Home: Vipi katika upande wa mavazi, unapendelea kutoka vipi?
Madee: Viwalo, mimi napenda sana kuvaa T-Shirt na ÔjnsiÕ.
Mpaka Home: Vipi kuhusu kupanda daladala, unajichanganya au jina linakupa wakati mgumu, mpaka teksi?
Madee: Yaani, kwanza nime-miss sana daladala, lakini kwa hivi sasa nina usafiri wangu.
Mpaka Home: Ni kitu gani kilichokufurahisha sana katika maisha yako na kingine kukuumiza?
Madee: Nilifurahi sana siku mtoto wangu aliponiita baba, na niliumia sana nilipoachana na mpenzi wangu.
Mpaka Home: Hongera sana kwa kuitwa baba, mlee vizuri mwanao, mpe elimu ya ukweli kwani atakusaidia baadaye.
Madee: Nashukuru kwa usahuri, karibu tena siku nyingine.
KARIBU SANA
JE, WEWE NI MJANJA?
UNAJUA KUDANSI?
SHOUT OUT !!
Followers
My Blog List
-
-
-
-
SIMBA SC. YAWEKA SOKONI MAJI YAKE!8 years ago
-
-
HARD PRICE COMING SOON10 years ago
-
-
-
Aslay Akifanya Vitu vyake13 years ago
-
-
-
-