ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU



"Nilifurahi sana siku ya kwanza kuitwa baba"

Baada ya kucheki bonge la ‘intavyuu’ kuhusu maisha ya mwanamuziki kutoka kiumeni Chegge, wiki iliyopita, Mpaka Home bado inaendelea kusonga mbele kiubishi na kufanikiwa kuyabamba maisha mapya ya mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Hamad Ali 'Madee' a.k.a Rais wa Mazese ambaye ni memba namba wani wa familia ya Tip Top Connection.
Hapo awali tuliwahi kumtoa mchizi huyu ambaye alikuwa bado akipiga ‘life’ flani nyumbani kwao, hivyo baada ya kuhamia kwake akiwa na umri wa miaka 28 sasa, Mpaka Home imetimba kwenye makazi yake mapya, Kimara- Rombo ili kujua mengi zaidi kuhusu laifu yake cheki na intavyuu hapo chini.

Mpaka Home: Mambo Madee?
Madee: Mambo mzuka tu, karibu sana maskani.
Mpaka Home: Nashukuru sana, ila ningependa kujua unaishi na nani hapa?
Madee: Hapa nipo na washikaji zangu wananipa kampani.
Mpaka Home: Mimi nilidhani kwa kuwa umehamia makazi mapya utaniambia uko na wifi yangu?
Madee: Hapana, bado nipo nipo kwanza.
Mpaka Home: Lakini si ulikuwa na demu Madee?
Madee: Ah! Yule si alinizingua mambo flani hivi.
Mpaka Home: Sasa inakuaje katika upande wa kupika, ukizingatia huu ni mwezi wa futari?
Madee: Mimi hapa nasubiria ikifika midamida tu nachukua tambi zangu naingia zangu jikoni.
Mpaka Home: Ni tofauti gani unaiona ulipokuwa nyumbani na sasa upo kwako?
Madee: Tofauti kubwa sana, kwa maana unapokuwa nyumbani huwezi kufikiria kufanya maendeleo yako, lakini ukiwa kwako kama hivi, unajituma hata kununua sofa.
Mpaka Home: Ni kitu gani unapenda kufanya unapokuwa nyumbani?
Madee: Napenda kufanya kazi zangu kwenye Kompyuta na kupiga gitaa langu.
Mpaka Home: Wanaume wengi hawapendi kujifulia, hususani mastaa, vipi kwa upande wako?
Madee: Mimi nafanya kila kitu mwenyewe, wala hilo halinisumbui kichwa sista.
Mpaka Home: Ni msosi gani unapenda kujipikia Madee?
Madee: Napenda sana kupika wali, haunisumbui kwa sababu natumia Rice Cooker.
Mpaka Home: Vipi katika upande wa mavazi, unapendelea kutoka vipi?
Madee: Viwalo, mimi napenda sana kuvaa T-Shirt na ÔjnsiÕ.
Mpaka Home: Vipi kuhusu kupanda daladala, unajichanganya au jina linakupa wakati mgumu, mpaka teksi?
Madee: Yaani, kwanza nime-miss sana daladala, lakini kwa hivi sasa nina usafiri wangu.
Mpaka Home: Ni kitu gani kilichokufurahisha sana katika maisha yako na kingine kukuumiza?
Madee: Nilifurahi sana siku mtoto wangu aliponiita baba, na niliumia sana nilipoachana na mpenzi wangu.
Mpaka Home: Hongera sana kwa kuitwa baba, mlee vizuri mwanao, mpe elimu ya ukweli kwani atakusaidia baadaye.
Madee: Nashukuru kwa usahuri, karibu tena siku nyingine.

Sunday, September 6, 2009 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "CHEKI MAISHA YA RAIS WA MANZESE"

Write a comment