Kutoka pande za TMK, mchizi ambaye anaedelea kusimama vyema ndani ya Kundi la Wanaume Family, Said Juma a.k.a Chegge Chigunda au Mtoto wa Mama Said amesema na ShowBiz kwamba kupitia programu inayoendelea ndani ya gazeti ndugu na hili, Risasi anajiandaa kupata mke wa maisha yake.
Msanii huyo (katika picha kubwa) alisema kwamba programu hiyo yenye jina la 'Shinda kuwa mke wa Chegge' imemkutanisha na wasichana wengi lakini anaamini atampata mmoja ambaye ni mwema. Kupitia programu hiyo msichana ambaye atashinda kuwa mke wa Chegge atatajwa wiki ijayo.
Hivi sasa Chegge amesimama na ngoma mbili, hewani, Karibu Kiumeni aliyomshirikisha Ngwea na Running Low remix aliyogonga na Wahuu wa Kenya, siku kadhaa zijazo ataachia kali nyingine, aliyompa shavu Lady Jaydee, unajua ni ipi? Kaa tayari

Friday, September 18, 2009
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "CHIGUNDA ANASUBIRI WAIFU"