ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Katika kusheheresha tuzo za MTV Afika zinazotarajiwa kutolewa mwezi ujao pande za Kenya, mchizi anayefanya vyema na ngoma kadhaa hivi sasa, Dapo Daniel Oyebanjo a.k.a DÕBanj kutoka Nigeria anatarajiwa kudondoka Bongo hivi karibuni kama mgeni mwalikwa kunako shoo yenye jina la Road to MTV Africa Music Awards (MAMA) itakayopigwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas Oktoba 3, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mratibu wa ishu hiyo, Christina Mosha 'Seven' shoo hiyo ambayo hufanyika kila mwaka na sehemu tofauti yakiwa ni maandalizi ya kuelekea kunako tuzo hizo safari hii itafanyika Bongo ambapo mbali na mkali huyo kutoka Nigeria pia wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania 'awadi' hizo Ambwene Yesaya 'A.Y' na Sara Kaisi 'Shaa' wataangusha burudani ya ukweli.
"Pia msanii kama Profesa Jay ambaye atakuwa ni mgeni mwalikwa katika tuzo hizo tutakuwa naye katika shoo hiyo ya Bilicanas ambayo itaanza saa tatu usiku na kuendelea kwa kiingilio cha shilingi 15, 000 kila mtu. Kwa ishu zaidi watu wanaweza kutembelea website yetu ambayo ni www.mama.mtvbase.com," alisema Seven.
Pia mratibu huyo amewaomba Watanzania na wapenzi wa burudani kwa ujumla wanaombwa kuendelea kuwapigia kura A.Y na Shaa ili waweze kuleta heshima Bongo kwa kuibuka na tuzo hizo. 'Kumpigia kura A.Y andika neno BHH AY kisha unatuma kwenda namba 0789 777 333. Ili kumuwezesha Shaa ambaye anawania tuzo ya Msanii Bora Anayechipukia andika neno BNA SHAA kisha tuma kwenda namba 0789 777 333.

Wednesday, September 23, 2009 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "D'BANJ KUDONDOKA BONGO"

Write a comment