Kupitia safu ya 'Mwana mpotevu' inayopatikana pia ndani ya gazeti la Ijumaa ShowBiz tutakuwa tukiwatafuta mastaa wa kitambo ambao waliwahi kufanya vyema kupitia sanaa zao kisha wakapotea. Kubwa zaidi litakuwa ni kwanini wapo kimya na huko waliko kwa wakati huo wanapiga ishu gani.
Kwa kuanza leo tunadondoka na binti aliyeingia kwenye game ya muziki wa kizazi kipya akiwa na umri mdogo na kufanya kazi kadhaa kisha kupotea, namzunguzia Doreen Mkude a.k.a Queen Doreen.
Alikuja kwa kasi na kushaini katika anga ya Bongo Flava kwa michano lakini ghafla ikawa jiiiii! Alipokutana na ShowBiz katikati ya wiki hii kabla ya yote alitamka kwamba sasa anarudi kamili kuwashika fans wote wa muziki.
Queen Doreen ambaye alikuwa memba active wa Kundi la Dar Scandal lililokuwa likiongozwa na Godfrey Tumaini 'Dudubaya', ameweka kweupe some issues zilizomfanya awe out of game kwa muda.
Mdada huyo alisema kuwa sababu namba moja iliyomfanya awe nje ya game ni masomo na kueleza kwamba aliona muziki Bongo si uwanja sahihi wa kuutegemea kufanya maisha ndiyo maana aliichenga Bongo Flava na kutimkia skonga.
Hata hivyo, Queen Doreen alisema kuwa kitu kingine kilichomkimbiza ni rushwa ya ngono kwa maelezo kuwa wadau wengi walikuwa wanabana kumsaidia mpaka pale atakaporidhia kuchekiwa on bed.
Mbali na hilo, aliimegea kona hii exclusive kwamba yupo anajiandaa na ujio mpya kwamba albamu yake ipo njia moja. Ni hayo tu kuhusu Doreen kwa leo. Cheki na sisi next week.
MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI
9 hours ago
One Responses to "QUEEN DOREEN BACK AGAIN"