ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Mkubwa akitunisha misuli
Afande akiwa na jazba
Mgogoro unaochukua nafasi pana kwa sasa katika kiwanda cha Bongo Flava ni kuhusiana na Mfalme wa Rhymes anayeendelea kudumu, Suleiman Msindi a.k.a Afande Sele na Meneja wa TMK Wanaume Family, Said Fella a.k.a Mkubwa.
Ishu iko hivi, ebwanadaah ilipiga stori na mastaa hao kwa nyakati tofauti ambapo wa kwanza alikuwa Sele aliyesema kuwa Mkubwa amekuwa akimfanyia kitu kibaya kwa kutaka kumpoteza kwenye game.
"Fella hanipendi, nikifanya shoo na Wanaume mara nyingi ananizimia MIC au anakorofisha mitambo ili sauti yangu isisikike vizuri. Fella hanipendi na mimi najua hilo," alisema Sele.
Akijibu hoja, Mkubwa alisema kuwa anasikitishwa na kauli za Afande na kwamba hakuna ukweli katika hilo na kuongeza kwamba ingekuwa vema mfalme huyo anayetokea pande za Moro akataja shoo ambazo alimzimia vyombo.
"Mimi naangalia mafanikio na maendeleo ya wasanii wa kundi langu, si kuendekeza roho mbaya kwa wengine," alisema Mkubwa.
Bifu ni hilo, nani mkorofi? Kama una data zimwage kupitia namba 0715-110 173 au mcgeorge2008@gmail.com.

Tuesday, September 29, 2009 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "MKUBWA FELLA, AFANDE ULINGONI!"

Write a comment