Studio mpya na ya ukweli iliyopo pande za Mburahati, Dar es Salaam, Apex Records imeanza kushika kasi, hivi sasa tayari imemsimamisha 'dogo' aliyekuwa anapiga kazi ndani ya kundi la 'Wachaji Zote', Heri Wilbad a.k.a Mtoto wa Binti Makombora ambaye hivi sasa anasikika na ngoma yenye jina la 'Niambie nijue' iliyogongwa na prodyuza Villy studioni hapo.
"Unajua baada ya kutengana na mshikaji kila mtu aliamua kusafa kivyake, hatimaye mimi nikashitukia nimeibukia Apex ambapo nipo lebo na tayari nimeshafanya ngoma hiyo na nyingine zinakuja chini ya prodyuza Villy ambazo kiukweli zitaniweka juu", alisema Mchaji.
Mbali na Mchaji, wasanii kibao wa muziki wa kizazi kipya wakiwemo TMK Wanaume Family wameshaanza kuibuka pande hizo na kufanya kazi kadhaa.
MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI
9 hours ago
One Responses to "APEX RECORDS YAANZA NA MCHAJI"