ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Baada ya kudondoka pande hizo alifanyiwa wellcome party na wenzetu
Akawapa shoo ya kiushikaji kabla ya kuingia mzigoni Alhamisi wiki hii
Ukifika sehemu kama hizi lazima upate picha za kumbukumbu unaweza usirudi tena huku


Msanii Ambwene Yesaya A.Y ambaye alikwea pipa mwishoni mwa wiki iliyopita kuelekea Malaysia tayari ameshadondoka pande hizo na jana Alhamisi aligonga shoo ya funiko kunako Jiji la Kuala Lumpur.
Akipiga stori na ebwana daah kwa njia ya simu kutoka pande hizo jamaa alisema kwamba kila kitu kuhusu ziara yake hiyo kimekwenda fresh na kwamba anatarajia kurudi Bongo Jumapili ya wiki hii kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wa kuwania tuzo za MTV Afrika kama Msanii Bora wa Hip Hop akichuana na mastaa kama Jay-Z na Kanye West.
Ili kumuwezesha kuibuka na ushindi A.Y andika neno BHH AY kisha tuma kwenda namba 0789 777 333. Ili kumuwezesha Shaa ambaye anawania tuzo ya Msanii Bora Anayechipukia andika neno BNA SHAA kisha tuma kwenda namba 0789 777 333

Wednesday, September 23, 2009 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "A.Y NDANI YA MALAYSIA"

Write a comment