Ishu mpya iliyodondoka pande hizi za ebwanadaah kutoka kwa Rais wa Manzese a.k.a Madee ambaye bado yupo kwenye majonzi ya kutosha kufuatia kifo cha mpenzi wake, inasema kwamba hivi sasa jamaa ameamua kutulia na kuandika kitabu kitakachoweka wazi mambo yake kibao likiwemo hilo la msiba.
“Mimi na Pendo tulipanga mambo mengi, aliwahi kuniambia malengo yake ni kusoma zaidi na baadaye kuwa mlezi wa watoto yatima. Lakini zaidi nitayaweka kwenye kitabu changu ambacho pia kitakuwa na full stori ya maisha niliyopitia mpaka nilipofika leo,” alisema.