Staa wa Bongo Flava, Zainab Lipangile ‘Zay B’ ameibuka na kuweka plain kwamba, lile bifu liliwahi kugonga vichwa kati yake na mwanamuziki mwenzake, Happy Thadei ‘Sister P’ bado liko pale baada ya kuwepo evidence kuwa still hawaivi in the same pot.
Akipiga stori na safu hii, jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Zay B alidai kwamba hawezi kuwa in a good understanding na Sister P pamoja na kwamba walishajaribu kuwa close, lakini wakaja kuhitilafiana tena na sasa uhusiano wao ni sifuri.
“Sitomsamehe Sister P milele kwa vitendo alivyonifanyia, hivi sasa anajifanya hana bifu na mimi lakini inawezekana moyoni mwake hayuko hivyo. Hivi sasa akifanya intavyuu na baadhi ya vyombo vya habari anawaambia yupo katika mishemishe za kurekodi na mimi na kwamba tumeshakutana tukaongea, kitu ambacho siyo kweli, hata akija na Rais Obama siwezi kufanya naye kazi,” alisema Zay B ambaye alitambulishwa na ngoma yake yenye jina la Gado, kabla Sister P hajatoka na ‘Anakuja’ kunako miaka ya 2002.
Zay B na Sister ni wasanii wa kike wa long time katika Tasnia ya Bongo Flava ambao some years huko nyuma waliwahi kuwa na bifu kali na kauli ya Zay B inayotoa tafsiri kuwa bado mtiti uko palepale. Safu hii itaendelea kucheki na Sister P ili kujua kama bado ndoto zake za kurekodi na Zay B ziko pale pale.

Monday, March 1, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "SISTER P, ZAY B BADO MOTO"