ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Master J akicheki ninavyowajibika kuandaa moja ya page za burudani

Muda mwingi alionesha kufurahishwa na kazi niliyokuwa naifanya

Baada ya ziara hiyo niliagana na Master J


Siku moja iliyopita nilipata zali la kutembelewa na Prodyuza galacha in Bongo Music, Joachim Kimaryo ‘Master J’ na kufanya naye interview katika maeneo kadhaa muhimu. Akiwa ofisini kwetu, Sinza, Bamaga, Dar es salaam mchizi alipata fulsa ya kujionea jinsi tunavyoandaa magazeti yetu mpaka yanawafikia wasomaji. Jay ambaye ni mmoja wa Maprodyuza walioishep Bongo Fleva wakati inasimama na kukubalika pamoja na aina nyingine ya muziki, alizungumzia mambo yafuatayo.

Mosi, alielezea BSS, pili ni kuhusu Bongo Fleva ilipotoka na inapokuja na tatu ni yanayohusu studio yake, lebo na wasanii anaowasimamia kwa jumla.

Kuhusu BSS, Jay alisema kwamaba, washindi wa taji hilo linaloheshimika kwa Watanzania hivi sasa, hawaoneshi cheche sokoni kwa sababu hawawezi kuandika.

Anasema: “Tatizo si BSS, Benchmark, Madam Rita wala majaji, tatizo ni wasanii wenyewe kwa sababu hawana uwezo wa kuandika na kuandaa nyimbo zao ili zikubalike.

“Wasanii wanaposhiriki BSS, wanaimba nyimbo za watu, kwahiyo wanaonesha uwezo wao kwa kuimba tu, hivyo wanakubalika na wanapigiwa kura lakini kwenye kutunga hakuna.

“Hii ndiyo sababu Jumanne Idd (mshindi mwaka 2007), Misoji Nkwabi (2008) wameishia njiani, unaona hata Pascal Cassian (2009) bado hajasimama, angalau Peter Msechu (1st runner up 2009) anaokoa jahazi.

“Nilitoa ofa ya wasanii wote walioingia Top 5 kurekodi nyimbo kwenye studio yangu (MJ Production) ili kuonesha mwanga ili Watanzania waone kwamba kumbe inawezekana Staa wa BSS akawa mfanyabiashara mzuri wa muziki nchini.

“Hilo tumeliangalia kwa mapana na mikakati ya BSS mwaka huu ni pamoja na kutafuta watu watakaowaandikia nyimbo washindi na kuwachagulia ala, kwahiyo baada ya shindano wataingia studio na kufyatua mawe yenye akili”. Mengi zaidi endelea kuchungulia blog hii.

Sunday, March 21, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "MASTER J ANIIBUKIA OFISINI"

Write a comment