Ze Dudu
The long time Artist wa Bongo Flava, Godfrey Tumaini a.k.a Dudubaya’, ambaye hivi sasa anasimama vema na ngoma mpya yenye jina la Push Push juzikati alipiga stori na Abby Cool & MC George over the weekend na kuchana kwamba, machungu aliyonayo moyoni hivi sasa yanamfanya asikie kichefuchefu pale msanii chipukizi anapomuibukia kumuomba msaada.
Mchizi alisema kuwa, machungu hayo yanatokana na fadhila ‘mbovu’ anazozipata kutoka kwa baadhi ya mastaa wa muziki wa kizazi kipya ambao alijitahidi kuwasapoti mpaka wakatoka lakini mwisho wa siku wakaamua kumdis bila sababu.
“Hivi sasa nina machungu sana, kiasi kwamba ‘andagraundi’ akija kuniomba msaada nasikia kichefuchefu kwasababu mwisho wa siku wanakosa shukrani kama ilivyokuwa kwa Hamidu ambaye nilimkuta yuko darasa la pili lakini shule haendi kutokana na matatizo ya familia yake, nikajitahidi kumsomesha mpaka akamaliza darasa la saba, lakini mwisho wa siku nikaonekana sina maana kwake”, alisema Ze Dudu.
Mastaa wengine aliowataja kuwasapoti mpaka wakachomoka kwenye game ni pamoja na Afande Sele ‘Baba Tunda’ msanii wa kike, ‘Besta’, Sister P, Pig Black na Crew ya Mabaga Fresh ambayo aliisaidia kutengeneza ngoma yao ya kwanza, ‘Mtulize’ kabla hawajachukuliwa na P-Funk na kugonga Mtulize remix wakiwa na Nature.

Monday, March 1, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "ZE DUDU: NINA MACHUNGU ILE MBAYA"