ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU


Ishu mpya iliyodondoka pande hizi inawahusu mastaa wawili wenye majina in the Bongo Flava, Khamis Mwinjuma ‘FA’ na Ambwene Yesaya ‘A.Y’, wako hand in hand katika kusukuma gurudumu la maisha.

Akipiga story na ebwanadaah juzikati, FA alitoa bonge la surprise pale alipoweka plain kwamba, kwa sasa meneja wake ni A.Y ambaye yuko mbioni kumaliza masomo yake ya biashara yaliyokuwa yakimuweka tight.

Akiwa na three weeks only tangu arejee Bongoland from kiwanja, mtu mzima FA alisema na safu hii kuwa mapema next week ataanza project mpya na meneja wake ambayo wataipa title hapo baadaye.

“Project hiyo itafanyika ndani ya B-Hits Company chini ya maprodyuza Hermy B na Pancho,” alisema.


Sunday, March 14, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "A.Y NDIYO MENEJA WANGU- MWANAFA"

Write a comment