ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Didas
Didas & Chiller (kushoto)
Didas na mdau
Q Chiller

Kutoka pande za UK huyu hapa ni Didas, mwanadada wa Kibongo ambaye anaendelea kugfanya mambo makubwa nchini humo na Afrika kwa ujumla kupitia kampuni yake yenye jina la Didas Facion inayodili na promotion za fashions pamoja na wasanii wa muziki kutoka Afrika Mashariki.
Akipiga stori na ebwanadaah kwa njia ya simu kutoka Uingereza, Didas alisema kwamba, kampuni yake ambayo pia ina matawi Tanzania na Uganda imewahi kupiga kazi na mastaa wa Kibongo kama Bushoke, Matonya, Q chillah, bendi ya FM Academia na wengine.
"Didas Facion yenye umri wa miaka nane sasa ilianza kazi zake rasmi 2002, wakati huo ikidili zaidi na dawa za kupunguza unene na afya kwa ujumla na ilijulikana kama Didas Health Care. Mwaka 2005 tuliamua kubadilika na kujitupa kwenye ishu za Fashions na Promotions za wasanii kazi ambayo tunaifanya mpaka sasa," alisema Didas.
Mrembo huyo alisema kwamba, mpaka sasa Didas Fashion inamiliki baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongo Flava, yaani Q Chiller, The blind sound, na Clipstar. "Siku za nyuma Didas Facion ilikuwa inamiliki wasanii zaidi ya 24 wakiwemo underground ambao baada ya kulipiwa studio na kufanikiwa kurekondi kazi zao wakaingia mitini. Tuliamua kuachana na chipukizi hao na kubaki na hao watatu
wakiongozwa na Q Chillah."
Kazi kubwa inayofanywa na Didas Facion hivi sasa ni kumrudisha Q Chiller kwenye game baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu. Kitakachofuata hivi karibuni ni ziara ndefu za Chiller nchi za nje, kama Europe, America na Africa ya mbali.
Kiukweli Didas ni mwanadada ambaye anastahili kuigwa na wanawake wote duniani kwani anajituma katika kutafuta maisha na anayependa maendeleo ya watu wengine kitu ambacho kinamfanya aendelee kufanikiwa.

Tuesday, November 30, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "DIDAS FACION MWANADADA WA KIBONGO ANAYEFANYA MAKUBWA UK"

Write a comment