Binti Mtanzania anayeiwakilisha Bongo kimasoma na kupiga game ya muziki wa kizazi kipya nchini Maylasia, Jesica Shayo a.k.a Jaymah au Sweety amedondoka Bongo kwa mapumziko mafupi kabla ya kurudi nchini humo kuendelea na shule pamoja na sanaa.
"Nimerudi kama wiki moja iliyopita, kilichonileta Bongo ambapo ndiyo home ni kuja kuhani msiba wa baba yangu mdogo ambaye alifariki hivi karibuni, lakini pia nitapata muda wa mapumziko kabla ya kuondoka tena," alisema Jaymah ambaye tayari ameshafanya ngoma kibao zikiwemo Best Frienda, Want You Know, Your Body, Forever na nyingine.
Sunday, November 21, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "JAYMAH ADONDOKA BONGO"