Kwa niaba ya Backyard Studio naomba nitoe tena fulsa ya pekee kwa Wasanii wote nchini iwe vikundi au mmoja mmoja kurecord nyimbo BURE kuanzia tarehe 30/11/2010 hadi tarehe 09/12/2010. Nyimbo hizo ziwe mahususi kwa ajili ya kusaidia, kuhamasisha jamii na kuelimisha kuhusu janga la Ukimwi linalo tukabili.
Dhumuni la Backyard kwa sasa ni kusaidia Jamii katika Majanga yote ya kitaifa kwa kupitia Sanaa. Tunaamini Ukimwi ni moja ya Janga kubwa sana linalo pelekea Serekali na Jamii kutumia pesa nyingi, muda na maarifa katika kutaka kuokoa maisha ya ndugu na jamaa zetu sambamba na kutokomeza gonjwa hili. Wasanii ni watu muhimu sana na naamini wakiamua kupiga kampeni hii ujumbe utafika na yote haya yana wezekana.
Naomba nyimbo ziwe za kweli zenye uwezo wa kukaa kwa muda mrefu zaidi na ambazo zitavutia jamii kusikiliza na ujumbe kuwafikia pale walipo ndani ya kipindi chote si wakati wa maadhimisho haya tu.
Tuwasiliane ili tupeane utaratibu wa kufuata japo hakuna mashari. Ahsante
Braton (Backyard Records)
S.L .P 14663 D'Salaam
Tanzania
+255 713 888 779.
One Responses to "HABARI NJE KUTOKA BACKYARD RECORDS"