About Me
MC Logo
PHOTOS
SHOW BIZ HITZ
BONGO HITZ
OLD SCHOOL FLAVA
Blog Archive
-
▼
2010
(208)
-
▼
September
(23)
- KOFI LA P-FUNK KWA AFANDE SELE
- MPYA KUTOKA KWA AFANDE SELE
- KAMA UNAMILIKI GARI UNAHUSIKA HAPA
- KID BWOY APUMZISHWA ICU
- MPAKA HOME KWA KINA MONICA
- SMS KUTOKA KWA MKUBWA FELLA
- BIFU LA MLELA, HEMED WADAU WAWASHAURI
- HOTPOT FAMILY KIVINGINE ZAIDI
- AFANDE, FEROUZ, MKOLONI STEJINI NA SUGU LEO
- UJIO MPYA WA HOTPOT FAMILY
- JAMANI, TUNAELEKEA WAPI?
- MIAKA 14 YA KIFO CHA TUPAC
- HUYU NDIYE MISS TANZANIA 2010
- Z-ANTO ARUDI STEJINI TIP TOP
- EID MUBARAK HOMIE
- TIP TOP KUMALIZA KAZI LEO
- KALA NA STAILI MPYA YA RANGI MBILI!
- P DIDDY WA MAIMARTHA AFARIKI DUNIA
- SAKATA LA K-SHER NA TIP TOP
- LINEX AITETEA NGOMA YAKE
- TABIA ANAWAZIMIA WANAUME HAWA
- WAPE USHAURI MLELA, HEMED
- MPAKA HOME KWA JERRY MURO
-
▼
September
(23)
G5 WORLD
ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU
"Mambo vp kaka? Maoni yangu leo kama mpiga kura, mzalendo na msanii mkubwa ni haya hapa. Viongozi wa dini wasikimbilie kwa MUNGU kuomba amani wakati huu wa uchaguzi bali wanatakiwa wawaambie Tume ya Uchaguzi wasijaribu kuchezea kura za watu kwa kutaka kumbeba mtu au chama chochote mahali ambapo hakikubaliki. Wakifanya hivyo mwaka huu nina hakika amani itavunjika wala maombi kwa MUNGU hayatasaidia na bila shaka itakuwa kama Kenya, kitu ambacho kitafanya viongozi wa Tume ya Uchaguzi na wa Serikali wakutane na mkono wa sheria katika Mahakama ya Kimataifa 'The Heque' chini ya Moreno Ocampo. Siyo kila jambo Wa-TZ tumsingizie MUNGU au shetani wakati tunasababisha wenyewe kwa tamaa za UFISADI wa baadhi ya watu. Tukifanya uchaguzi huru na wa haki daima huwa na amani lakini wizi wa kura, udanganyifu na kuchakachua matokeo ndiyo sababu kubwa ya vita, uasi na matatizo katika taifa lolote"
Read More......Kutoka pande za Rock City (Mwanza), mtayarishaji muziki aliyekumbwa na balaa la kuumizwa na mtu asiyejulikana akiwa ndani ya studio yake na kulazwa katika Hospitali ya Bugando, Sandu George Mpanda a.k.a Kid Bwoy amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’.
Akipiga stori na kipindi cha Michano Time kinachorushwa na Kituo cha Radio Passion FM cha Mwanza, chini ya mtangazaji wake Phillbert Kabago katikati ya wiki hii, baba mdogo wa Kid Bwoy, Jose Mpanda alisema kwamba mgonjwa wao amehamishiwa ICU ili kumpa muda mzuri wa kupumzika tofauti na alipokuwa kwenye wodi ya kawaida.
“Napenda kuwatoa wasiwasi ndugu, jamaa na marafiki wa Kid Bwoy kwamba mgonjwa wetu anaendelea vizuri, lakini madaktari wamelazimika kumuhamishia kule kwasababu ya kumpa muda mzuri wa kupumzika. Unajua aliopokuwa amelazwa wodini watu wengi walikuwa wakija kumuona huku wengine wakitumia muda mrefu zaidi kitu ambacho kilikuwa kikimfanya apate muda mchache wa kupumzika,” alisema Jose.
Baba mdogo huyo wa Kid pia alisema kwamba, pamoja na mgonjwa wao kujitambua na kuanza kuongea, wameombwa na dokta anayemshughulikia wasimuulize maswali mengi hasa kuhusiana na tukio zima hadi pale afya yake itakapotengemaa zaidi. Kid alikumbwa na mkasa huo Jumatano ya wiki iliyopita saa 2 usiku akiwa ndani ya studio yake yenye jina la Tetemesha Records. ShowBz inampa pole za kutosha, inaendelea kumuombea apone haraka ili arudi katika hali yake na kulisukuma gurudumu la muziki wa Bongo Flava.
Kutoka ndani ya kiwanda cha muvi Bongo, wiki hii Mpaka Home imedondoka na kipaji kinachokuj kasi kunako mradi huo, namzungumzia mwanadada Monica Malaki aliyeuza kupitia filamu ya Hot Friday.
Mengi kuhusu yeye na maisha yake kwa ujumla chungulia intavyuu ya kijanja hapo chini.
Mpaka Home: Sema Monica, historia yako kwa ufupi ikoje?
Monica: Nilizaliwa mwaka 1988 Moshi, Kilimanjaro, nampenda mama yangu mzazi kuliko vitu vyote.
Mpaka Home: Vipi kuhusu suala zima la elimu?
Monica: Niliishia kidato cha nne tu baada ya kupata elimu ya msingi hapa hapa Dar es Salaam.
Mpaka Home: Lini uliingia katika tasnia ya muvi Bongo?
Monica: Niliingia mwaka 2004, ila niliibuka zaidi 2008 kupitia filamu ya ‘Hot Friday’ kwani nilipigiwa simu kibao za pongezi kwa kazi nzuri.
Mpaka Home: Nani aliyegundua kipaji chako?
Monica: Vicent Kigosi ‘Ray’, binafsi namshukuru sana maana ndiye aliniita na kunieleza kwamba nina kipaji cha kuigiza.
Mpaka Home:Kwa sasa mashabiki wako wategemee nini kutoka kwako?
Monica: Kuna filamu kibao ambazo nimecheza na wakali mbalimbali ambazo zinakuja kuwakimbiza.
Mpaka Home: Unaweza hata kuzitaja chache?
Monica: Hapana,siwezi kwa sasa..ila wakati muafaka ukifika nitazitaja.
Mpaka Home: Nje ya kuigiza unafanya nini?
Monica: Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) ambapo nachukua Stashahada ya Masoko nikiwa mwaka wa pili.
Mpaka Home: Unautumiaje muda wako huku katika kuigiza filamu na wakati huo huo unasoma?
Monica: Napenda sana kusoma na napenda sana kuigiza, hivyo muda wa kusoma ni wa kusoma na muda wa filamu ni wa filamu.
Mpaka Home: Lakini ni vigumu kuwatumikia mabwana wawili?
Monica: Ndio maana nimekuambia kwamba kila kitu na muda wake, sio kwa wakati mmoja.
Mpaka Home: Vipi una mpenzi?
Monica: Nikose mpenzi tena…miye !
Mapaka Home: Kwanini usikose mwaya?
Monica: Ninatatizo gani? Kwa kifupi ninaye ila hayuko hapa nchini kwa hivi sasa.
Mpaka Home: Yuko wapi na anaitwa nani?
Monica: Yuko nchini Italia kibiashara, nisingependa kumtaja kwa jina kwa sasa, mpaka baadaye kidogo.
Mpaka Home: Nije lini kuchukua jina lake?
Monica: (Anacheka) Aaaah! Bado muda ukifika hata mimi mwenyewe nitakutafuta ili nikutajie.
Mpaka Home: Ulishawahi kuachwa?
Monica: Sijawahi ila mimi n’shawatosa wengi wenye mapenzi ya kuigiza.
Mpaka Home: Unamaanisha nini unaposema mapenzi ya kuigiza?
Monica: Aaah bwana wee nani anataka mapenzi ya kudanganyana? Mimi nikiona mtu simuelewi elewi namtosa tu.
Mpaka Home: Vipi, jamaa ndio yuko kiwanja huku nyuma mapedeshee hawakusumbui kukutaka kimapenzi?
Monica: Mimi ni mtoto wa kike, nakwambia wapo hata vigogo ambao wananitokea lakini najitambua pamoja na kuwepo kwa vishawishi kibao lakini napenda kutumia msemo wasasa ‘SIDANGANYIKI’.
Mpaka Home: Unaweza kumwanika hadharani hata kigogo mmoja anayekufukuzia ili liwe fundisho kwa wengine?
Mpaka Home: Unajua kupika?
Monica: Utakimbia…. Unaweza kujing’ata vidole
Mpaka Home: Wazazi wako ni wapande za wapi?
Monica: Wanaishi Mbezi ila asili yetu ni Kilimanjaro
Mpaka Home: Wasanii wengi wa kibongo hasa chipukizi huteswa na rushwa ya ngono pale wanapotaka kupewa nafasi ya kuigiza, vipi wewe ulishawahi kupatwa na mkasa kama huu?
Monica: Ni kweli lakini kwa bahati mbaya sijawahi kukumbwa na mkasa huu.
Mpaka Home: Unasemaje kuhusu tasnia ya filamu hapa Bongo?
Monica: Ni ngumu, kikubwa ni kukaza msuli ili kuweza kuliteka soko la filamu.
Mpaka Home:Tunashukuru sana Monica kwa ushirikiano wako
Monica: Asanteni sana, karibuni tena.
Read More......Miss TZ 2010, Genevieve Emmanuel Mpangala (katikati) akiwa na mshindi wa pili, Glory Mwanga (kushoto) na mshindi wa tatu, Consolata Lukosi mara baada ya kutangazwa washindi juzi kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam
Read More......IKIWA KATIKA MUONEKANO MPYA BAADA YA KUBORESHWA BLOG YAKO YA KIJANJA, ebwanadaah INAWATAKIA WAISLAMU NCHINI KOTE SIKUKUU NJEMA YA EID NA KUWAOMBA WASHEHEREKEE KWA AMANI NA UTULIVU KAMA ILIVYO DESTURI YETU.
KARIBU SANA
JE, WEWE NI MJANJA?
UNAJUA KUDANSI?
SHOUT OUT !!
Followers
My Blog List
-
-
-
-
SIMBA SC. YAWEKA SOKONI MAJI YAKE!8 years ago
-
-
HARD PRICE COMING SOON10 years ago
-
-
-
Aslay Akifanya Vitu vyake13 years ago
-
-
-
-