ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Kutoka pande za Rock City (Mwanza), mtayarishaji muziki aliyekumbwa na balaa la kuumizwa na mtu asiyejulikana akiwa ndani ya studio yake na kulazwa katika Hospitali ya Bugando, Sandu George Mpanda a.k.a Kid Bwoy amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’.

Akipiga stori na kipindi cha Michano Time kinachorushwa na Kituo cha Radio Passion FM cha Mwanza, chini ya mtangazaji wake Phillbert Kabago katikati ya wiki hii, baba mdogo wa Kid Bwoy, Jose Mpanda alisema kwamba mgonjwa wao amehamishiwa ICU ili kumpa muda mzuri wa kupumzika tofauti na alipokuwa kwenye wodi ya kawaida.

“Napenda kuwatoa wasiwasi ndugu, jamaa na marafiki wa Kid Bwoy kwamba mgonjwa wetu anaendelea vizuri, lakini madaktari wamelazimika kumuhamishia kule kwasababu ya kumpa muda mzuri wa kupumzika. Unajua aliopokuwa amelazwa wodini watu wengi walikuwa wakija kumuona huku wengine wakitumia muda mrefu zaidi kitu ambacho kilikuwa kikimfanya apate muda mchache wa kupumzika,” alisema Jose.

Baba mdogo huyo wa Kid pia alisema kwamba, pamoja na mgonjwa wao kujitambua na kuanza kuongea, wameombwa na dokta anayemshughulikia wasimuulize maswali mengi hasa kuhusiana na tukio zima hadi pale afya yake itakapotengemaa zaidi. Kid alikumbwa na mkasa huo Jumatano ya wiki iliyopita saa 2 usiku akiwa ndani ya studio yake yenye jina la Tetemesha Records. ShowBz inampa pole za kutosha, inaendelea kumuombea apone haraka ili arudi katika hali yake na kulisukuma gurudumu la muziki wa Bongo Flava.


Friday, September 24, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "KID BWOY APUMZISHWA ICU"

Write a comment