Mlela
Hemed
Baadhi ya wadau wa sanaa ya muvi bongo waliyoguswa na bifu la wasanii wawili, Yusuf Mlela na Hemd wamedondosha maoni yao wakiwashauri vijana hao ambao wamekuwa wakilumbana kupitia baadhi ya vyombo vya habari, huku wakitishia kuchapana makonde. Zaidi kuhusu maoni hayo cheki hapo chini.
Kadole wa Dar : Mimi nadhani anachokifanya Hemed ni kama ushamba , katika hali ya kawaida huwezi kujisifu mbele ya chombo cha habari kuwa umempiga fulani ngumi. Kwa hili nahisi hakuwa sawa.
Baba Calvin wa Kinondoni Dar : Hawa vijana walitakiwa kutumia busara zaidi kuamua suala lao kwani walinavyokashifiana kupitia vyombo vya habari wafahamu kwamba hata soko la filamu zao wanalichafua. Kama wanaweza bora wawe na wasemaji wao wenye uwezo wa kuchambua jambo la kuongea, ni aibu kwa tukio kama hilo, nathubutu kusema hakuna staa wala supa staa kati yao.
Saida wa Mwanza: Mimi nalipongeza gazeti la Ijumaa kupitia hapa ShowBiz kwa kuliona hilo. Ushauri wangu kwao nawataka kwanza watambue umuhimu wao kwenye jamii, pia watambue kuwa wanatazamwa na watu wengi, wakubwa kwa watoto, hivyo waache bifu zisizokuwa na maana.
Kulwa wa Temeke, Dar: Mlela na Hemed wote siyo mastaa, kati yenu hakuna anayemfikia Kanumba wala Ray. Badala ya kufanya kazi ili mzidi kupaa kisanii mnaanza kutuletea bifu zenu za ajabu, nyie bado ni chipukizi sana fanyeni kazi acheni hizo.
Mussa wa Kilwa Masoko: Hemed unajifanya unajulikana Afrika nzima kwa kipi? Acheni majigambo, nyie bado mna safari ndefu kwenye sanaa hamuwezi kuwafunika wakongwe kwa staili hiyo.
Kalunde wa ILALA, Dar: Nadhani hao jamaa hawajijui kama ni kioo cha jamii, nawashauri waende kwa madaktari kucheki vichwa vyao, kwa maana hadhi waliyonayo kama ni wazima kweli hawawezi kufanya ishu kama hizo za kurushiana maneno machafu kwenye vyombo vya habari.
Mama Idd wa Kigamboni, Dar: Nyie vijana wote ni kioo cha jamii, tumieni busara badala ya kuanza kutukanana ovyo. Hivi mnadhani watoto watajifunza nini kutoka kwenu? Acheni hizo.
Light wa Moro: Namshauri Mlela aachane na bifu kwani anashusha heshima yake katika jamii kwakuwa yuko juu na anajitahidi katika sanaa.
Manyama wa Musoma: Hao wote hakuna staa kati yao kwani tumeshajua hiyo ni janja yao tu ya kujitafutia umaarufu, zaidi wanataka kutujaribu akili zetu.
Paparazi Venance wa Dar: Kama mnafikiri kazi ya sanaa inaboreshwa kwa kuwa na bifu basi Kibongobongo mnajiharibia, hakuna jipya mnalolileta kwetu zaidi ya kutuzingua. Fanyeni kazi, acheni bifu zenu zisizo na malipo, hii Bongo msitake kujifananaisha na akina Kanye na 50 Cent nyie bado andagraundi.
Kumbukeni ya Mr. Nice na Dudubaya walivyojimaliza kwa ugomvi wao.
Friday, September 17, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "BIFU LA MLELA, HEMED WADAU WAWASHAURI"