"MAMA HALIMA NI NGOMA YANGU, SIYO YA KIDUMU"
Stori iliyopo kitaani hivi sasa ni kuhusu ngoma ya msanii Sunday Mangu a.k.a Linex inayokwenda kwa jina la ‘Mama Halima’ ambayo imekuwa ikiwachanganya mashabiki wengi wakidhani ni wimbo wa Kidumu wa Kenya, kisa sauti zinarandana.
Akiangusha stori na ShowBiz juzi kati, Linex alisema kwamba ngoma hiyo ambayo hivi sasa iko juu imekuwa ikimpa wakati mgumu na kumfanya aonekane mwenye majonzi kwani baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiiomba redioni kwa jina la Kidumu.
“Napenda kuwaambia kwamba ‘Mama Halima’ ni ngoma yangu, ili kuepusha utata uliojitokeza tayari nimepiga kideo ambacho kitaanza kuonekana siku kadhaa zijazo. Ngoma hiyo pia imebeba jina la albamu yangu ambayo itadondoka kitaa hivi karibuni ikiwa na nyimbo 13,” alisema.
Mchizi pia aliwataja ‘maproducer’ waliohusika kuwa ni Villy wa 24/7 Records, Prof. Ludigo, Tuddy, Solomoni Lamba, Jala Man, Dunga na Lamar, pia amewapa shavu wakali kibao wa Bongo Flava.
Friday, September 3, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "LINEX AITETEA NGOMA YAKE"