Home kwake
Tunzo alizowahi kupata
Jikoni
Akichukua juisi
Akiperuzi kwenye mtandao
Seating room
Nje ya nyumba yake
Akijipumzisha
"Naomba Watanzania waniombee kwa sababu napita katika kipindi kigumu sana kwenye maisha yangu"
“Nilizaliwa January 17, 1980, hapa hapa Dar, ni mtoto wa pili kati ya watano tuliozaliwa kwa mzee Murro. Kaka yetu wa kwanza anaishi Marekani, wengine tuko hapa nchini.
“Nilipata elimu yangu ya msingi pale Ubungo NHC, baadaye sekondari ya Loyola ambako nilisoma mpaka kidato cha nne, kidato cha 5 na 6 nilisoma Lutheran Junior Seminary. Baada ya hapo ilifuatia elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako nilichukua Degree ya Sayansi ya Siasa na Utawala 2003-2006, kisha nikaenda , South Afrika nilikochukua mambo ya Mabunge ya Africa 2006, baadaye Sweden nilikosomea masuala ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007, nikamalizia Merekani ambako nilikwenda kuchukua Utawala Bora na Rushwa mwaka 2008.”
Huyo ni Mwanahabari Jerry Cornel Muro aliyetokea kujipatia umaarufu wa kutosha pamoja na kutunukiwa tuzo kadhaa ikiwemo ile ya Mwandishi Bora wa habari za uchunguzi na ndiye staa aliyefuatwa na Mpaka Home ‘Next Level’ mwishoni mwa wiki iliyopita na kuweka wazi kuhusu maisha yake kwa sasa.
Pande za Kunduchi, Dar es Salaam ndiko anakofanya maisha yake ndani ya mjengo wake wa kisasa, Mpaka Home ilipofika nyumbani hapo majira ya jioni ilimkuta jamaa amejipumzisha, huku akisoma Gazeti ndugu na hili, Ijumaa. Kilichofuata baada ya salamu za hapa na pale ilikuwa ni intavyuu, cheki nayo hapo chini.
Mpaka Home: Tangu tumefika hapa kwako sijaona dalilia yoyote ya kuwa na mwanamke ndani ya nyumba hii, ina maana bado hujachukua jiko?
Muro: Bado sijaoa lakini nipo kwenye uhusiano.
Mpaka Home: Nani anakusaidia kazi za upishi hapa nyumbani?
Muro: Mimi mwenyewe, huwa napika chakula cha aina yoyote.
Mpaka Home: Unapendelea zaidi chakula gani?
Muro: Wali kwa maharage yaliyoungwa kwa nazi au ndizi kwa nyama.
Mpaka Home: Ni vitu gani ambavyo hauvipendi katika maisha yako?
Muro: Sipendi umaskini, kuona wananchi wakionewa na dhuluma.
Mpaka Home: Kitu gani ambacho unakipenda zaidi?
Muro: Kuwatumikia wananchi, na kuona kila mtanzania anapata fursa ya kumiliki uchumi na kuwa na maisha bora.
Mpaka Home: Kipindi hiki ambacho uko nje ya kazi kutokana na matatizo ya kesi yako, muda mwingi unautumia kufanya nini?
Muro: Nakua hapa nyumbani kama ulivyonikuta, najipanga upya.
Mpaka Home: Unajipanga upya kivipi?
Muro: Nikiwa nyumbani nautumia muda wangu kuandika baadhi ya ishu zangu kwenye kompyuta na kupumzisha akiri baada ya dhoruba ili la kesi.
Mpaka Home: Mwisho unawaambiaje wasomaji na wapenzi wa safu hii?
Muro: Nawaomba Watanzania waniombee kwa sababu napita katika kipindi kigumu sana kwenye maisha yangu.
Mpaka Home: Tunashukuru kwa ushirikiano wako Jerry.
Muro: Asanteni, karibuni tena.
Mpaka Home inapatikana ndani ya Gazeti la Risasi Jumatano litokalo kila siku hiyo.
Thursday, September 2, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "MPAKA HOME KWA JERRY MURO"