Hatumwi mtoto dukani Mbeya, wana wa Uyole, Mafiati,Mwakibete, Mwanjelwa, Isanga, Nzovwe, Soko Matola, Ghana, Majengo na mitaa mingine ya jiji hilo, macho na fikra zao ni sehemu moja tu usiku wa leo. Ni ndani ya Ukumbi wa Mtenda Sunset.
Kunani? Jibu ni kwamba Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, leo anaweka kando gwanda na kuvaa jeans na baada ya hapo atasomeka katika shoo kali ya Hip Hop lakini atasindikizwa na wana wengine wa muziki wa kizazi kipya.
Sugu a.k.a Mr. II, atapiga mzigo mkali kuthibitisha ukongwe wake wa zaidi ya miaka 20 kwenye MIC, atasimama jukwaani zaidi ya saa nzima akikamua shoo ya kweli ya Hip Hop, lakini watakaoingia ukumbini pia wataburudika na Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, Ferouz Mrisho Rehani, Abbas Hamis Kinzasa ’20 Percent’, Danny Msimamo, Fred Maliki ‘Mkoloni’, Gerald Mwanjoka ‘G Solo’, Mapacha ‘Maujanja’ na Isanga Family’.
Akifafanua kuhusu kupanda jukwaani na kuvua kombati ya CHADEMA, Sugu alisema nasi kuwa anafanya hivyo leo, ikiwa ni onesho maalum la kukusanya michango ya kampeni.
“Leo gwanda pembeni, navaa jeans na kushika MIC. Jukwaa moja na Afande, Ferouz, Mkoloni, 20 Percent, Msimamo, Isanga Family na wengine. Ni shoo maalum ya kuchangia kampeni. Tumegawa kadi maalum ambapo kuna maeneo zinanunuliwa kama njugu. Kila kadi tunauza shilingi 10,000.”
Thursday, September 16, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "AFANDE, FEROUZ, MKOLONI STEJINI NA SUGU LEO"