Kutoka ndani ya mradi wa muvi Bongo, mwanzoni mwa wiki hii ShowBiz ilipata chansi ya kugonga stori mbili tatu na staa wa game hiyo ambaye pia aliwahi kutwaa mataji kadhaa ya urembo nchini , Tabia Batamwanya ambaye alifunguka kwamba anawahusudu sana wanaume weusi na wenye nguvu.
Tabia aliiambia blog hii kwamba wanaume kibao wamekuwa wakimtokea kila kukicha lakini amekuwa akiwaonesha msimamo wake kwamba yeye siyo ‘demu’ wa kumkubali kila ‘men’ anayekuja usoni kwake ukizingatia kwamba tayari anaye ampendae.
“Wengi wakiniona kwenye muvi au kwenye muziki wanadhani wanaweza kunidanganya nikakubali, mimi siko kiihivyo japo siku zote nimekuwa nikivutiwa na wanaume weusi, ambao wako ‘strong’, siyo legelege,” alisema.
Kwa upande wa game ya muvi tayari mwanadada huyu ameshapiga filamu tatu, huku moja yenye jina la Babla ikiwa kitaani. “Kwa upande wa muziki pia bado naendelea kulisongesha, lengo ni kufika mbali zaidi katika sanaa na kujiongezea kipato, sitaki kuwa msanii wa kuuza sura bila mafanikio,” alisema Tabia.
Friday, September 3, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "TABIA ANAWAZIMIA WANAUME HAWA"