ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU







Kutoka ndani ya kiwanda cha muvi Bongo, wiki hii Mpaka Home imedondoka na kipaji kinachokuj kasi kunako mradi huo, namzungumzia mwanadada Monica Malaki aliyeuza kupitia filamu ya Hot Friday.

Mengi kuhusu yeye na maisha yake kwa ujumla chungulia intavyuu ya kijanja hapo chini.


Mpaka Home: Sema Monica, historia yako kwa ufupi ikoje?

Monica: Nilizaliwa mwaka 1988 Moshi, Kilimanjaro, nampenda mama yangu mzazi kuliko vitu vyote.

Mpaka Home: Vipi kuhusu suala zima la elimu?

Monica: Niliishia kidato cha nne tu baada ya kupata elimu ya msingi hapa hapa Dar es Salaam.

Mpaka Home: Lini uliingia katika tasnia ya muvi Bongo?

Monica: Niliingia mwaka 2004, ila niliibuka zaidi 2008 kupitia filamu ya ‘Hot Friday’ kwani nilipigiwa simu kibao za pongezi kwa kazi nzuri.

Mpaka Home: Nani aliyegundua kipaji chako?

Monica: Vicent Kigosi ‘Ray’, binafsi namshukuru sana maana ndiye aliniita na kunieleza kwamba nina kipaji cha kuigiza.

Mpaka Home:Kwa sasa mashabiki wako wategemee nini kutoka kwako?

Monica: Kuna filamu kibao ambazo nimecheza na wakali mbalimbali ambazo zinakuja kuwakimbiza.

Mpaka Home: Unaweza hata kuzitaja chache?

Monica: Hapana,siwezi kwa sasa..ila wakati muafaka ukifika nitazitaja.

Mpaka Home: Nje ya kuigiza unafanya nini?

Monica: Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) ambapo nachukua Stashahada ya Masoko nikiwa mwaka wa pili.

Mpaka Home: Unautumiaje muda wako huku katika kuigiza filamu na wakati huo huo unasoma?

Monica: Napenda sana kusoma na napenda sana kuigiza, hivyo muda wa kusoma ni wa kusoma na muda wa filamu ni wa filamu.

Mpaka Home: Lakini ni vigumu kuwatumikia mabwana wawili?

Monica: Ndio maana nimekuambia kwamba kila kitu na muda wake, sio kwa wakati mmoja.

Mpaka Home: Vipi una mpenzi?

Monica: Nikose mpenzi tena…miye !

Mapaka Home: Kwanini usikose mwaya?

Monica: Ninatatizo gani? Kwa kifupi ninaye ila hayuko hapa nchini kwa hivi sasa.

Mpaka Home: Yuko wapi na anaitwa nani?

Monica: Yuko nchini Italia kibiashara, nisingependa kumtaja kwa jina kwa sasa, mpaka baadaye kidogo.

Mpaka Home: Nije lini kuchukua jina lake?

Monica: (Anacheka) Aaaah! Bado muda ukifika hata mimi mwenyewe nitakutafuta ili nikutajie.

Mpaka Home: Ulishawahi kuachwa?

Monica: Sijawahi ila mimi n’shawatosa wengi wenye mapenzi ya kuigiza.

Mpaka Home: Unamaanisha nini unaposema mapenzi ya kuigiza?

Monica: Aaah bwana wee nani anataka mapenzi ya kudanganyana? Mimi nikiona mtu simuelewi elewi namtosa tu.

Mpaka Home: Vipi, jamaa ndio yuko kiwanja huku nyuma mapedeshee hawakusumbui kukutaka kimapenzi?

Monica: Mimi ni mtoto wa kike, nakwambia wapo hata vigogo ambao wananitokea lakini najitambua pamoja na kuwepo kwa vishawishi kibao lakini napenda kutumia msemo wasasa ‘SIDANGANYIKI’.

Mpaka Home: Unaweza kumwanika hadharani hata kigogo mmoja anayekufukuzia ili liwe fundisho kwa wengine?

Mpaka Home: Unajua kupika?

Monica: Utakimbia…. Unaweza kujing’ata vidole

Mpaka Home: Wazazi wako ni wapande za wapi?

Monica: Wanaishi Mbezi ila asili yetu ni Kilimanjaro

Mpaka Home: Wasanii wengi wa kibongo hasa chipukizi huteswa na rushwa ya ngono pale wanapotaka kupewa nafasi ya kuigiza, vipi wewe ulishawahi kupatwa na mkasa kama huu?

Monica: Ni kweli lakini kwa bahati mbaya sijawahi kukumbwa na mkasa huu.

Mpaka Home: Unasemaje kuhusu tasnia ya filamu hapa Bongo?

Monica: Ni ngumu, kikubwa ni kukaza msuli ili kuweza kuliteka soko la filamu.

Mpaka Home:Tunashukuru sana Monica kwa ushirikiano wako

Monica: Asanteni sana, karibuni tena.

Wednesday, September 22, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "MPAKA HOME KWA KINA MONICA"

Write a comment