ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

"Kaka, pamoja na wa TZ wengi kuwa bize wakati huu wa mambo ya World Cup, ni vyema pia kama wakiwa bize katika kujua na kufuatilia Bunge wakati huu pia kwakuwa ndiyo wakati ambao Bunge limepitisha bajeti ya nchi. Na bila shaka bajeti ndiyo muhimu zaidi kwetu kwakuwa ndiyo muamuziki wa maisha na hatma ya taifa letu masikini.
"Wale wenzetu wanaocheza World Cup wanatambua hilo katika nchi zao na ndiyo maana wamefanikiwa kufika pale na kushiriki mashindano yale, michezo na burudani ni mambo ambayo yana maanisha furaha na starehe katika maisha ya mtu. Na ili mtu afurahi na kustarehe anatakiwa awe ameshapata vitu vyote muhimu na vya msingi katika maisha kama kula kupata elimu, matibabu, kufanya kazi na hata kuvaa na kulala.
"Baada ya kufanikiwa katika vitu hivyo vya msingi ndipo mtu anapoweza kuburudika na kucheza, hivyo ndivyo maisha yalivyo na ndivyo wafanyavyo wenzetu wenye kujielewa. Ni aibu kusikia eti wabunge wetu wanakacha vikao muhimu vya bajeti ya nchi kwa ajili ya kuangalia World Cup", Afande Sele.

Sunday, June 20, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "AFANDE: NI AIBU WABUNGE WETU KUKACHA VIKAO KWASABABU YA WORLD CUP"

Write a comment