Pia kama ulikuwa haujafahamu, kuna bonge la ishu limedondoka pande hizi, 'ebwanadaah' likitengeneza kichwa cha habari kisemacho kwamba, A.Y kupiga kolabo na Sean Kingston, ikiwa na maana kwamba siku kadhaa zijazo mchizi atakwea pipa na kwenda kupeperusha bendera ya Bongo katika nchi ya Obama kwa kufanya kazi na staa huyo.
Picha lilianzia ndani ya kituo cha Redio Cloud FM pale Sean Kingston alipokuwa anafanyiwa ‘intavyuu’ kupitia kipindi cha XXL muda mchache baada ya kuwasili Bongo kwaajili ya shughuli nzima ya utoaji tuzo za Kili iliyofanyika hivi kariubuni.
Ndani ya ‘intavyuu’ hiyo ambayo ilirekodiwa kwenye video ya Frank Mtao wa 2Eyez Production, Sean Kingston alisema kwamba msanii wa Bongo anayemkubali zaidi ni A.Y na kwamba alitamani kuangusha naye kolabo, kitu ambacho kiliwafanya wasaidizi wake wawasiliane na Mzee wa Commercio ambaye alipata ‘chansi’ ya kukutana na staa huyo kisha kubadilishana mawazo.
“Nilipokutana na jamaa kweli alisema anavutiwa na kazi zangu, akaniomba tukapige kolabo, ni mtu ambaye hana mapozi na ilikuwa nipige naye ngoma moja hapa Bongo lakini bahati mbaya prodyuza wangu, Hermy Bakawa amesafiri. Kwa kifupi amenipa moyo sana, nikienda huko natarajia kufanya maajabu,” alisema A.Y .
One Responses to "UJUMBE KUTOKA KWA A.Y"