Hapa jamaa walipoangusha burudani Kanda ya Ziwa

Hapa nikimkaribisha Shumba, kiongozi wa Makhirikhiri aone jinsi ninavyopiga mzigo


Hapa nikishoo lavu na mwanadada Linda wa Makhirikhiri


Mdau Walter a.k.a Mcharuko (katikati) ye alikuwa bize na kina Shumba tu

Hapa mimi na Wafanyakazi wenzangu wa Global Publishers tulipata fulsa ya kupiga picha ya pamoja na Makhirikhiri
Siku moja iliyopita mimi pamoja na wafanyakazi wa Kampuni yetu ya Global Publishers tulipata bahati ya kutembelewa na kundi maarufu la muziki wa asili kutoka Botswana, Makhirikhiri linaloongozwa na Moses Malapela a.k.a Sumba Ratshega na kupiga nao stori mbili tatu.
Baada ya kuacha gumzo Kanda ya Ziwa kwa shoo kadhaa za ukweli, jamaa wanatarajia kuacha historia Bongo kwa kupiga kazi ya nguvu ndani ya Ukumbi Diamond Jubilee Ijumaa ya wiki hii kwa kiingilio cha buku 20 kwa VIP na buku 10 kawaida. Mimi pia ntakuwepo kwasababu nawakubali ile mbaya, wewe je?
Friday, June 4, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "USO KWA USO NA MAKHIRIKHIRI"