ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU



Kundi la muziki wa asili kutoka Botswana, Matsuwe Tradition Dance maarufu kama Makhirikhiri bado lipo Bongo na kinachofuata hivi sasa ni ziara mkoani Mbeya ambapo litaangusha shoo ndani ya Uwanja wa mpira wa Sokoine Juni 12, mwaka huu kabla ya kumalizia Iringa katika Uwanja wa Samora.
Sisi kama ShowBiz leo tunamcheki kiongozi wa kundi hilo, Moses Malapela ambaye ana a.k.a ya Shumba Ratshega. Wengi hawajui Shumba katoka wapi mpaka kufikia hapa alipo leo kama kiongozi wa kundi la Makhirikhiri mwenye sauti ya kipekee katika ngoma za muziki huo wa asili.
Mchizi alizaliwa 1981 katika kijiji cha Bobonong, nchini Botswana ni miongoni mwa wasanii wa muziki huo waliopitia pilikapilika za hapa na pale. Alianza kama mcheza shoo ndani ya Kundi la Re Tlaa Re Ke Dipitse Cultural Group lililokuwa hapo hapo kijijini kwao.
Baada ya hapo alijimuvuzisha hadi kwenye kundi lingine lililokuwa na jina la Motswedi Cultural Group. Jina la Shumba alilipata kupitia kabila yao, Kalanga likiwa na maana ya Simba huku lile la Ratshega kwa mashabiki wake alipokuwa akipiga shoo.
Alitoa albamu yake ya kwanza kama muimbaji na mchezaji mwaka 2006 ikiwa na jina la Masiela. Albamu hiyo ambayo haikumtambulisha vyema ilifuatiwa na Makhirikhiri 2007 ambayo ilifanya vizuri na kuuzwa katika nchi kibao zikiwemo Botswana yenyewe, Afrika Kusini, Namibia, Zambia na Zimbabwe.
Mwaka huo huo wa 2007, kupitia Tuzo zenye jina la Mascom-Bomu Awards, Makhirikhiri aliibuka na ushindi kama albamu bora ya asili. Mwaka 2008 Shumba aliitambulisha albamu mpya yenye jina la Ntopolela Bichana kupitia wimbo wa Dikhwaere. Mwaka jana wa 2009 akatambulisha albamu nyingine yenye jina la Kukantsu.
Kupitia muziki wake, Shumba ameweza kujiwekea heshima ndani na nje ya nchi yake Botswana, mfano mzuri ni pale alipofanya shoo mbele ya rais wao, Lt General Seretse Khama Ian Khama kwenye sherehe za uhuru na kuwaburudisha mawaziri wote wa nchi hiyo kwenye hafla ya chakula cha usiku.
Akiwa na kundi lake, Makhirikhiri, Shumba amewahi kufanya shoo Afrika Kusini, China, Namibia, Zambia na Angola kabla ya kuja Tanzania. Kutokana na heshima aliyoijengea nchi yake kabla hajaja Tanzania, Rais wao, Lt General Seretse Khama Ian Khama alimkabidhi bendera kwa ajili ya kuitangza zaidi Botswana.

Friday, June 11, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "A-Z KUHUSU SHUMBA WA MAKHIRIKHIRI"

Write a comment