ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU


Kutoka pande za Rock City kijana SAJNA anayekuja juu kunako game ua miziki wa kizazi kipya amedondoka ndni ya jiji la Dar kwa ishu ya kuitangaza album yake ya kwanza ambayo iko katika hatua za mwisho kukamilika na kwamba inatarajiwa kutelemka sokoni mwezi mmoja ujao.
"Album itakwenda kwa jina la IVETA, itakuwa na jumla ya ngoma kumi zikiwemo IVETA, BINADAMU, MBALAMWEZI, SUBIRA, MGANGA, ROHO MBAYA, NADHIFA na nyinguine. Katika album hii atawashirikisha BELLE 9, LINAH na JOSEFLY, lengo la kuwapa shavu wasanii hao wachache ni kutaka kuonesha kipaji chake zaidi.
Studio zilizohusika kuigonga album hii ni pamoja na TETEMESHA RECORDZ (Kid bwoy), AB RECORDS (Amba), MUSIC LAB (Duke), MZUKA RECORDS (Benja) na A2P RECORDS (Sam Timba)," alisema Kid Bwoy.

Friday, June 11, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "HUYU NDIYO SAJNA, ADONDOKA DAR"

Write a comment