ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU


Jaffarai (kushoto) na Mox

Kutoka pande za Kijitonyama, Dar mchizi aliyewahi kufanya vyema kupitia ngoma yenye jina la ‘Napenda nini’, Jaffari Ally Mshamu a.k.a Jaffarai amesema na ebwanadaah kwamba ‘Demu wangu’, ngoma yake inayofanya vyema hivi sasa tayari imetupiwa kwenye kamera za video na muda wowote inaanza kuuza kunako vituo kadhaa vya televisheni.
Akipiga stori zaidi, Jaffarai alisema kwamba video ya ngoma hiyo imefanyika sehemu kadhaa ndani ya Dar es Salaam chini ya mtayarishaji John Kallage huku ikiwauzisha sura mastaa kibao wa Bongo flava na wadau wa muziki huo ambao ni kipenzi cha msanii huyo.
“Bado naamini kuwa ili msanii afanye kazi nzuri hata kama ni mkongwe lazima aumize kichwa kwa kuandika kazi nzuri, ndiyo maana mimi niko ‘bize’ kuhakikisha kila ngoma ninayotoa inakuwa juu kama hii “Demu wangu’ niliyomshirikisha TID ambaye hakufanya masihara kwenye korasi,” alisema Jaffarai.

Friday, June 11, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "JAFFARAI AMUWEKA DEMU WAKE KIDEONI"

Write a comment