ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU


Aliyekuwa staa wa muziki wa Kiafrika kutoka pande za Gaboni, Oliver N’goma amefariki dunia katika Hospitali ya Omar Bongo iliyopo Libreville huko huko Gabon. Kwa mujibu wa mtandao mwanamuziki huyo aliaga dunia juzi Jumatatu akiwa na umri wa miaka 51.
Olive N'goma a.k.a Noli alizaliwa Machi 23, 1959 pande za Mayumba, Mashariki wa Gaboni akiwa katika familia ya wanamuziki. Ndani ya game ya muziki alikuwa na uwezo mkubwa wa kuandika mashairi, kuimba na kucharaza gita, kazi iliyomfanya akatambulika karibu ulimwengu mzima ilikwenda kwa jina la Bane ambayo aliiachia 1989. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amen.

Wednesday, June 9, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "OLIVER N'GOMA AFARIKI DUNIA"

Write a comment