Mwanadada aliyetengeneza jina kupitia shindano la kufatuta vipaji, Bongo Star Search 2008, Beatrice William, kupitia ebwanadaah amedondosha ushauri wake kwa shindano hilo kwamba hivi sasa wanatakiwa kuangalia mshiriki gani ambaye ana uwezo wa kuandika na kuimba nyimbo zake mwenyewe.
Msanii huyo kutoka pande za Mwanza ambaye hivi sasa anafanya vizuri na ngoma yenye jina la ‘Acha waone’ alifunguka hayo baada ya kuulizwa na safu hii anadhani ni kitu gani kinachowafanya washindi wa BSS washindwe ‘kushaini’ katika game ya muziki.
“Binafsi nadhani umefikia wakati sasa kwa waandaaji na wapiga kura kuangalia nani mwenye uwezo wa kutunga na kuimba, siyo mwenye uwezo wa kuimba nyimbo za watu wengine kama ilivyokuwa kwenye mashindano yaliyopita kitu ambacho kimewafelisha washindi kwakuwa wanashindwa kuandika nyimbo zao,” alisema Beatrice, ambaye kifamilia ni mama wa watoto 3.
Friday, July 30, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "BEATRICE ADONDOSHA USHAURI BSS"