ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Mashabiki wa Moro walivyoitikia wito
Tip Top Connection pia walikuwepo
Hapo nyuma, Jipanguse, Rraaaaaaaaaa!!!

Jipangusee, Rrraaaaaa!! Ndiyo kauli mbiu ya tamasha kubwa la Fiesta 2010 ambalo hufanyika mara moja kila mwaka na kuwakutanisha wasanii kibao kutoka ndani na nje ya Bongo.

Kwa mujibu wa waandaaji, Primetime Promotion, mwaka huu mpango mzima ulianzia pande za Morogoro Julai 7 na kuendelea pale Matongee Club, Arusha Julai 9 ikifuatiwa na Kilimanjaro Julai 10, wilayani Moshi ndani ya Club La Liga.

Baada ya Kilimanjaro shoo itahamia Dodoma, Tanga, kabla ya kurudi Dar es Salaam mwisho wa mwezi huu, kisha Zanzibar, Musoma na sehemu nyingine kibao.

Wasanii kama Mwasiti Almasi ‘Mwasiti’ anayefanya vyema na ngoma yake, ‘Siyo kisa pombe’, Diamond, Madee na wengine kibao ni miongoni mwa vichwa vitakavyosababisha shangwe za ‘Kujipangusa’ katika tamasha hilo la kijanja. Wote sema Rrrrraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!

Sunday, July 11, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "MORO WALIVYOANZA KUJIPANGUSA"

Write a comment