ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU


Leona akijiachia na mpenzi wake, Lou Al-chamaa

Kuanzia leo kupitia hapa nitakuwa nawadondoshea uhusiano wa mastaa mbalimbali wa kiwanja, yaani nani anajiachia na nani na aliwahi kuwa na uhusiano na nani. Kwa kuanza leo tunacheki na staa wa muziki wa R&B, Leona Lewis. Kama hujafahamu kuhusu maisha yake ya uhusiano, amewahi kutoka na mmoja tu ambaye ameweza kujulikana na kuwekwa wazi.

Lou Al-chamaa ndiye anayetajwa kwamba kuanzia mwaka 2002 mpaka sasa, wamekuwa pamoja na hakuna mwanaume yeyote aliyewahi kuweka chata zaidi ya jamaa huyo.

Hata hivyo, hivi karibuni kuna uvumi ulichukua nafasi kwamba wawili hao wameachana, ingawa hakuna kati yao aliyejitokeza na kuzungumzia taarifa hizo kama zina ukweli au ni longolongo.

Jina lake kamili ni Leona Lewis, umri wake ni miaka 25, urefu wake ni futi 5.7. Alizaliwa Aprili 3, 1985, Islington, London, Uingereza. Ebwana dah! Pia inapatikana ndani ya Gazeti la Ijumaa Wikienda litokalo kila siku ya J’tatu. Hakikisha ulikosi.

Sunday, July 18, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "EBWANA DAAAAAH!!"

Write a comment