Wengi wanaweza wakashangaa na kujiuliza inakuwaje? Lakini kwake iko poa tu kwakuwa ni muumini mzuri wa Dini ya Kiislam ndiyo sababu iliyomsukuma kugeukia pande hizo na kufanya kazi ya Mungu mpaka kukamilisha albamu yenye nyimbo nne za Kaswida ikiwa na jina la Mazingira.
Namzungumzia Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Hassan Fella ambaye amesema na ShowBiz kwamba, kila kitu anachofanya na kufanikiwa ni mapenzi ya Mungu ndiyo sababu kubwa iliyomfanya ageukia upande huo kwa kuwasaidia vijana wa Chuo cha Kiislamu chenye jina la Al-Madrasaty Salama kilichopo Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam.
“Mkubwa tumetoa albamu au Nashdi, inaitwa Mazingira ikiwa na Kaswida 4 ambazo ni Ndoa, Ukimwi, Rushwa na Mazingira yenyewe. Pia tumetoa na video yake ikiwa kwenye DVD na VCD kazi zote tunasambaza wenyewe, kwa mara ya kwanza tutazitambulisha Agosti mosi mwaka huu,” alisema Fella.
Friday, July 16, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "MKUBWA NDANI YA KASWIDA!"