Mchomvu na B-12 watakuwepooooo!!
Godzilla, Belle 9 ndani
Fiesta siyo burudani peke yake, pia inahusika katika kutoa misaada kwa jamii mbalimbali yenye matatizo kama anavyoonekana Kibonde akiwakilisha misaada kwa kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo pande za Arusha
Kiukweli hii picha ilinivutia ile mbaya. Kushoto ni jirani yangu Henry Mdimu na Chegge, bado sijafahamu walikuwa wanasheherekea Birhday ya nani walipokuwa kwenye ziara ya Fiesta Arusha!..Hebu nambie jamani.
Dodoma mko tayari kujipangusaaa!! Nalizungumzia Tamasha la Fiesta 2010 ambalo lilianza kupagawisha katikati ya wiki iliyopita pande za Morogoro, ikifuatiwa na Arusha na Moshi na sasa ni zamu ya watu wa Dodoma kuondoa matatizo yao kupitia shangwe hizo ambazo zitapigwa kesho ndani ya Uwanja wa Jamhuri.
Primetime Promotion ndiyo waandaaji, ndani ya safu hii wamesema kwamba kama ilivyokuwa sehemu nyingine zilizotangulia ndivyo itakavyokuwa Dodoma kwasababu huwa hawabahatishi na kwamba idadi ya wasanii watakaodondoka pande hizo itakuwa ya kutosha.
Baadhi ya wasanii waliotajwa kushuka Dom ni pamoja na Juma Nature, Fid Q, Keisha, Madee, Kassim, Tundaman, Johmakini, Bele 9, Barnaba, Mwasiti, Linah, Amini, Diamond, Godzilla, Roma, Niki wa Pili, Young Dee, Mataluma na wengine kibao. Baada ya pande hizo msafara utaelekea Tanga kwa shughuli kama hiyo huku timu ya wasanii ikizidi kuongezeka.
Waandaaji hao walisema kwamba, baada ya Tanga, mzigo utatua Zanzibar, kisha Kanda ya Ziwa kabla ya kurudi Dar na kuangusha burudani ya ukweli kwa shoo itakayopigwa kunako sehemu itakayotajwa hivi karibuni.
Friday, July 16, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "FIESTA DOM KESHO, RRAAAAA!!!"