Wacha waoneeee!! Betrice
Inawezekana ishu hii ikawa kama ‘sapraiz’ kwa wasomaji wengi wa ShowBiz au mashabiki wa msanii Betrice William ambaye ni zao la BSS 2009 aliyesimama katika game ya muziki wa kizazi kipya hivi sasa akiwa na ngoma yenye jina la ‘Acha waseme’ ikiwa pamoja na video yake.
Kama haujafahamu bado, mbali na kushiriki vyema kunako shindano la BSS na kuonesha uwezo mkubwa katika shoo zake, msanii huyo (picha kubwa katika pozi) ni mama wa watoto wa watatu ambao ni Milee, Abel na mdogo wao Vaines na kwamba yuko taiti na game ili kuhakikisha madogo hao wanapata mahitaji yote ikiwemo elimu.
Akipiga stori na ebwanadaah hii msanii huyo alitamka kwamba, haoni sababu ya kuficha kuwa ana familia kama ilivyo kwa mabinti wengine kwakuwa kwake anajivunia watoto na hata anapoonekana kuwa ‘tait’ na game ya muziki mashabiki wake watambue kwamba majukumu ndiyo yanampa mzuka zaidi wa kazi.
“Huwezi amini, nilijifungua mwanangu wa kwanza nikiwa na umri wa miaka 18, mpaka sasa nina miaka 28, kipindi chote hicho nilikuwa tayari kwenye game ya muziki, japo sikuwahi kutoka kama ilivyo sasa. Wanangu wapo kwa bibi yao (mama yake mzazi) Mwanza pande za Igogo wanaendelea na shule huku mimi na baba yao tukiendelea kuwasapoti kwa kila kitu,” alisema Beatrice.
Kuhusu game msanii huyo ambaye atakuwa mwenyeji wa tamasha la Fiesta 2010 pande za kwao, Kanda ya Ziwa alisema kwamba, baada ya kufanya vizuri na ngoma hiyo, Acha waseme siku kadhaa zijazo atasimamisha jiwe lingine kati ya mawili aliyokwisharekodi. “Zipo ngoma mbili, Dance floo na Ndiyo sababu ambazo nitazikabidhi kwa wadau ili wachague moja ambayo itakwenda hewani, naomba mashabiki wangu waendelee kunipa sapoti ili niongeze mzuka zaidi,”.
Friday, July 16, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "WATOTO WA BEATRICE HAWAMZUII KUFANYA GAME"