ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Katika kuonesha kwamba yuko ‘andastending’ na ile kauli mbiu ya kupambana na gonjwa hatari la Malaria ‘Zinduka’, mwanadada Khadija Shaban a.k.a K-sher alijikuta amejisogeza kwa daktari ili kujua kama kinachomsumbua ni ugonjwa huo au la.
Ishu hiyo ilichukua nafasi pande za Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita wakati mwanadada huyo anayefanya game ya muziki kupitia kundi la Tip Top Connection alipokuwa kwenye ziara ya tamasha la Fiesta inayoendelea hivi sasa hapa nchini.
“Unajua nilikuwana Malaria tangu wiki iliyopita nikapima na kupata dawa, lakini baada ya kufika Dodoma nikawa sijisikii vizuri ikabidi nikapime tena kwenye Hospitali Kuu ya Mkoa nikakutwa na Malaria 3, nikapewa dawa nyingine, hivi sasa nashukuru Mungu naendelea poa,” alisema K-sher.
ShowBiz inampa pole msanii huyo na inamuombea apone haraka ili aendelee kuwakilisha kupitia game ya muziki wake.
Maoni kuhusu K-Sher cheki na sisi kwa anuani zilizopo juu kulia.

Friday, July 23, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "K-SHER AZINDUKIA KWA DAKTARI DOM"

Write a comment