Mataluma na Temba wakishuka pande hizo
R.O.M.A na Belle 9 pia ndani
Linah, Amini live
Ule mpango wa kujipangusa, yaani ‘Rrraaaaaaaaa’ bado unaendelea na sehemu zinazofuata baada ya Tanga na Zanzibar ni Kanda ya Ziwa, Musoma na Mwanza.
Nalizungumzia Tamasha kubwa la Fiesta 2010 ambalo leo liko pande za Musoma huku timu ya wakali wa Bongo Fleva ikichukua nafasi stejini na kujiopangusa pamoja na maelfu ya mashabiki watakaojitokeza usawa huo.
Primetime Promotion ambao ni waandaaji wa mpango huo wa kujipangusa wamesema na ebwanadaah kwamba upande huo ishu nzima itachukua nafasi ndani ya Musoma Hotel huku wasanii kama Temba, Chegge, Belle 9, Barnaba, Linah, Beatrice William, Amini, Fid Q na wengine kibao wakisababisha kwa kuhakikisha burudani yote inakwenda sawia.
“Baada ya Musoma, kesho Jumamosi itakuwa ni zamu ya Mwanza kwa shoo ambayo itaanzia ndani ya Yatch Club na kufuatiwa na Uwanja wa CCM Kirumba Jumapili, huku msanii Fid Q akiwa ndiyo mwenyeji wetu,” walisema waandaaji.
Friday, July 30, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "MUSOMA, MWANZA JIPANGUSEEE!!!"