ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Ray C
Mwisho mjengoni BBA All Stars
Mwisho

Mwanadada Rehema Chalamila a.k.a Ray C leo anatokea tena hapa ebwana daah! akiwa na ishu mpya inayomuhusu yeye na ‘X Boyfriend’ wake, Mr. Morogoro a.k.a Mwisho Mwampamba ambaye bado anaendelea kula bata ndani ya mjengo wa Big Brother All Stars huko Sauzi.
Kama bado hujainyaka ishu yenyewe ni kwamba, mwanadada Ray C amefunguka na kumfagilia Mwisho huku akimtakia ushindi mwema katika shindano hilo la BBA kwani bahati kama hiyo huwa haiji mara mbili.
Akipiga stori na Dj Fetty kupitia kipindi cha Bongo Fleva kilichorushwa na kituo cha redio Clouds FM mwishoni mwa wiki iliyopita, Ray C alisema kwamba hakujisikia vibaya Mwisho alipomtaja kama girfriend wake wa zamani kwakuwa anazidi kumtangaza.
“Kwangu iko poa, yeye kunitaja BBA kwakuwa anazidi kunitangaza, ukizingatia kwamba mimi na Mwisho bado tunawasiliana kama marafiki. Kikubwa namtakia ushindi, ajitahidi kwa kuitumia nafasi hiyo aliyoipata mara ya pili vizuri ili arudi Bongo na pesa hizo,” alifunguka Ray C baada ya kuulizwa na Dj Fetty anajisikiaje kutajwa na Mwisho wakati akiingia kwenye mjengo wa BBA?

Friday, July 30, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "RAY C AMPA GWALA MWISHO BBA"

Write a comment