Baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu, hatimaye kijana Aboubakari Shaban Katwila a.k.a Q Chiller amerudi tena kwenye game, safari hii akiwa amejipanga kutoka kivingine lengo likiwa ni kupiga ishu kimataifa zaidi. Now ninavyokwambia tayari mchizi keshadondosh ngoma moja kideoni ikiwa na jina la Saba mara sabini ikiutambuliusha ujio wa albamu yake mpya itakayosomeka kama A Sing of Matureness. Kama haujafahamu bado mpango mzima kuhusu Chiller unasimiwa na mwanadada jasiri, Dida kupitia kampuni yake, Dida Fashion UK. Kuna mengi zidi kuhusu ujio wa Chiller, usicheze mbali na blog hii ya kijanja.
Sunday, July 18, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "CHILLER BACK AGAIN"