ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU


Kala na shemeji yetu

Hapa Kala (wa pili kutoka kushoto) akiwa na wana wa pande hizo

Kutoka pande za Uganda a.k.a UG, mwana Hip Hop wa Kibongo, Kala Jeremiah amesema na ebwana daah kwamba zaidi ya miezi miwili sasa yuko nchini humo akipiga madude ya ukweli ikiwa ni njia mojawapo ya kujipanga ili arudi kivingine na pia amefanikiwa kummiliki sista duu wa kona hizo za Museven.

“Niliondoka Bongo zaidi ya miezi miwili iliyopita baada ya kumpata mtu ambaye atasimamia kazi zangu fresh ambaye anaishi huku Uganda, kwa bahati nzuri pia nikafanikiwa kukutana na mrembo huyo ambaye nampenda kupita kiasi tukaanzisha uhusiano. Niliamua kufanya hivi baada ya kuumizwa na mademu wa Kibongo ambao kwangu nawaona kama wazinguaji,” alisema Kala.

Mchizi ambaye kimuziki alijulikana kupitia shindano la kusaka vipaji la BSS mwaka 2007 na kushika nafasi ya nne, alisema kwamba wasichana wengi wa Kibongo hawana mapenzi ya dhati zaidi ya kuweka mkwanja mbele kitu ambacho kinawafanya wasidumu na wanaume.

“Mimi pia nilikuwa nashangaa, hapo Bongo nilikuwa na bahati ya kupata wasichana wazuri lakini sikuwahi kudumu nao, naamini huyu wa huku baadaye anaweza kuwa mke wangu wa milele,” alisema Kala ambaye alikiri kuwa kila akifikiria kurudi nyumbani Tanzania mrembo huyo ambaye hakumtaja jina anahisi kama anamzuia kwa jinsi alivyompenda.


Sunday, July 11, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "KALA HANA HAMU NA MADEMU WA KIBONGO"

Write a comment