ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Monica katika pozi
...hapa akiwa na shoga yake, Brandy (kulia)

...hapa akijiachia na mbwa wake

Safu yako ya kijanja, Ebwana Dah! Wiki hii inakudondoshea majina ya mastaa wa kiume waliowahi kufanya mapenzi na staa wa R&B pande za US, Monica Arnold. Kwa mujibu wa site ya kiwanja ambayo ipo serious katika kufuatilia uhusiano wa mastaa hasa wa kwa himaya ya Obama, Usher Raymond ndiye anatajwa kuwa mwanaume wa kwanza wa Monica na inaelezwa kuwa walitoka mwaka 1995.
Jarvis Weems anatajwa kuwa wa pili na alichangamka naye kuanzia mwaka 1998 hadi 2003 lakini Monica akiwa kwenye uhusiano huo, mwaka 2000 alimegeka kisela kwa C-Murder.
Young Buck alifaidi penzi la Monica mwaka 2004 na mwaka 2005 akajituliza kwa Rodney Hill.
Jina lake kamili ni Monica Denise Arnold, alizaliwa Oktoba 24, 1980 College Park, Georgia, Marekani. Umri wake ni miaka 29 na ni mhitimu wa High North Clayton High School, Atlanta, Georgia. Safu hii pia inapatikana ndani ya Gazeti la Ijumaa Wikienda linalotoka kila siku ya Jumatatu.

Sunday, July 25, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "EBWANA DAAH! WIKI HII"

Write a comment