Chiller katika muonekano mpya
Ishu mpya kutoka kwa staa wa ngoma ya ‘Tutaonana wabaya’ Aboubakari Shaban Katwila a.k.a Q Chiller iliyodondoka pande hizi wiki hii inasema kwamba hivi sasa mchizi hataki kusikia habari za kushirikishwa (kolabo) katika ngoma za wasanii wengine.
Akipiga stori na blog hii chini ya meneja wake, Khadija Seif wa Dida Fashion UK, Chiller alisema kwamba hivi sasa hataki kusikia habari za kushirikishwa kwasababu yuko tait na ujio wake mpya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu.
“Hivi sasa nipo kwenye mishemishe za kwenda levo nyingine, sihitaji kushirikishwa na msanii yoyote, nimeshawasaidia sana kilichopo mbele yangu muda huu ni kuangalia jinsi ya kuupeleka muziki wangu mbali,” alisema.
Akiwa ametoka chimbo na ngoma yenye jina la Saba mara sabini inayofanya vizuri sasa, jamaa pia yuko tayari kulitaja jina la albamu yake mpya ambayo ni A sing of matureness kwakuwa tayari imeshakamilika kinachofuata ni video za ngoma kadhaa kabla ya kuwapelekea walaji. Kama una maoni kuhusu Chiller cheki na sisi kwa anuani zilizopo juu.
Friday, July 23, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "Q CHILLER KUZIPOTEZEA KOLABO"