Akiwa amepitia milima, mabonde na vikwazo kibao mpaka kufikia mafanikio aliyonayo leo, mwanadada Judithi Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee yuko tayari kusheherekea miaka kumi tangu aingie kwenye game ya muziki wa kizazi kipya kunako miaka ya 2000.
Mwanadada anayo kila sababu ya kusheherekea kwakuwa tangu ajitupie kwenye fani miaka kumi iliyopita, hajawahi kushuka chini au muziki wake kutosikika kwa muda mrefu kupitia vyombo mbalimbali vya habari tofauti na baadhi ya mastaa alioanza nao safari ambao hivi sasa hawajulikani walipo.
Uvumilivu na mishemishe alizogonga mpaka kufikia hatua ya kumili bendi yenye jina la Machozi vinaifanya a.k.a yake, Komando kuwa ya ukweli zaidi kwani ameonesha ni jinsi gani ni jasiri katika kupambana kwa kuipigania sanaa yake mpaka ikampeleka mbali.
Kupitia blog yake Jide amedondosha maneno yanayosomeka hivi. “Tarehe 6 August ni Show Kubwa ya Miaka 10 Ya Lady JayDee….chagueni nyimbo mnazopenda kuzisikia, nitajaribu kugusa kuanzia, Machozi, Binti, Moto, Shukrani na Album ya Combination ya Machozi Band”.
Kama bado haujafahamu ishu hiyo ita-take place pande zipi, mpango mzima utachukua nafasi Mzalendo Pub iliyopo ndani ya mjengo wa Millenium Tower, Makumbusho, Dar es salaam. Ebwana daah! ambayo ni mdau namba moja wa burudani Bongo inaungana na mwanadada Jide katika furaha yake ya kutimiza miaka kumi kwa mafaniko japo bado safari yake kimuziki inaendelea.
Friday, July 30, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "JIDE NDANI YA MIAKA 10"