ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Kalapina katika sura mbili tofauti

Kutoka kikosini Block 41, mwana-Hip Hop mwenye harakati zenye uzani mkubwa Bongo, Kalama Masoud ‘Kalapina’ amejitosa kwenye ulingo wa kisiasa ikiwa ni pamoja na kuweka wazi azma yake ya kugombea Udiwani wa Kata ya Kinondoni, Dar.
Kalapina ameitonya Ijumaa Showbiz kuwa dhamira yake ya kuwania udiwani kwenye kata hiyo ni kushirikiana vema na wananchi ili kuindeleza kata hiyo kwa huduma mbalimbali za kijamii, kiuchumi, pia kuendeleza harakati za vijana katika Mapinduzi ya Kisiasa.
“Nawaomba wananchi wenzangu waniunge mkono ili tuendeleze harakati, muziki kama kawaida siachi, nitafanya siasa na muziki pamoja. Ijulikane kuwa sikuingia kwenye siasa kwa kukurupuka, bali naijua, pia wazee wamenishauri nigombee kwa sababu nakubalika sana kwenye kata yetu,” alisema Kalapina na kuongeza:
“Nagombea kwa tiketi ya CUF, mimi ni mwanachama wa CUF tangu mwaka 1999. Nataka nimpumzishe diwani wa sasa Michael Lupiana kwasababu siasa ya siku hizi inahitaji vijana wenye uwezo wa kusimamia mambo, kujenga hoja, kubuni na kutekeleza masuala yenye manufaa kwenye jamii, sifa ambayo mimi ninayo.”

Read More......
Friday, February 26, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Kumpeneka katika pozi tofauti

Baada ya kupotea kwa takribani siku kadhaa, staa wa ngoma ya Dk. Wangu, Salum Kumpeneka ‘Dr. Kumpeneka’, ameibukia ndani ya blog hii na kuchana kuwa siku chache zijazo ataibuka tena kunako game ya muziki wa kizazi kipya akiwa chini ya Poteza Records inayomilikiwa na Said Fella a.k.a Mkubwa.
Akiwa anapiga kazi na prodyuza, Suesh, Kumpeneka ni miongoni mwa wasanii waliyopata bahati ya kuwa wa kwanza kusimamiwa na lebo hiyo chini ya mradi wenye jina la 'Mkubwa na wanawe'. Mengi zaidi kuhusu mchizi endelea kuchungulia blog yako ya kijanja, 'ebwanadaah'.


Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Cheki pozi za H. Baba
Hamis Ramadhani Baba a.k.a H. Baba mzee wa Poteza amesema na blog hii kwamba, baada ya kumbaini adui yake aliyetaka kumpoteza kwenye game kwa ishu za kishirikina sasa anasonga mbele na hafikirii tena kurudi nyuma kwakuwa tayari ameshapata matibabu nyumbani kwao Mwanza.

"Hivi sasa tayari nimeshakabidhi albamu kwa mdosi, ninachosubiri ni kugonga kopi tu. Kazi itakayotambulisha albamu hiyo yenye jina la Goma la Uswazi inaitwa Umeshaniumiza, ni poteza la ukweli ambalo litanirudisha kwenye game 2010. Mwaka ndo umeanza, nimejipanga vya kutosha ili kuhakikisha nasimama kama zamani.
"Albamu ina ngoma nane zikiwemo Goma la Uswazi iliyobeba jina, utanipa na nyingine kibao. Pia mashabiki wangu watakutana na vichwa kama Hussein Machozi, Omari Mkali, Tundaman na vingine kibao ambavyo nimevipa shavu," alisema H. Baba.



Read More......
Thursday, February 18, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Gabboman ndani ya pozi tofauti


Unamkumbuka Gabboman? Kama haujawahi kumsikia ni kwamba, mchizi alikuwa ndani ya kundi la Ragga bwayz kabla ya kujitoa na kuanza kupiga ishu kimpango wake ambapo alifanikiwa kutoka na ngoma kadhaa ikiwemo Mama wa Kambo, lakini hazikuweza kumtambulisha vyema. Ishu mpya iliyondoka ndani ya ebwanadaah siku chache zilizopita inasema kwamba, hivi sasa mshikaji amejipanga kurudi kivingine ili kuuanza mwaka huu wa 2010 kwa kasi mpya. Zaidi endelea kufuatilia blog hii ya kijanja.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Farida

Kabago
Farida (kushoto) akipozi na Kabago

Kutoka pande za Rock City a.k.a Mwanza, mchizi aliyepata kutamba na kundi lake la BWV la jijini humo, Phillibert Kabago ameweza kufanya mpango mzima wa kumrudisha Farida aliyepotea kwa miaka mingi kupitia ngoma yenye jina la 'Wivu' ambayo mwanadada huyo kaonesha uweza wa juu. Ngoma hiyo iliyofanyika kupitia Tetemesha Records tayari imeanza kufanya vyema kupitia vituo kadhaa vya redio huku maandalizi ya video yakiendelea.














Read More......
Wednesday, February 10, 2010 Posted in | | 0 Comments »


Comedian wa Kibongo, Babu Ayoub ambaye hivi karibuni ameibuka na staili yake ya kunywa bia kupitia chupa ya mtoto amegeukia kunako upande wa muziki wa taarabu na ishu iliyodondoka punde tayari ana mashabiki kibao kupitia ngoma yake yenye jina la 'Chaja ya Kobe'. Hivi ni kweli muziki wa kizazi kipya hivi sasa umefulia ndiyo maana wasanii wengi wanaamua kubadili upepo? Kama wewe unaijali Bongo Flava kama mimi hebu tujadili jinsi ya kuirudisha kwenye chati.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »




Msanii Jittaman (kushoto katika picha zote mbili) kutoka pande za Rock City wiki iliyopita alimdaka mmoja kati ya Wabongo wengi wenye tabia ya kuuza kazi feki za wasanii hasa wa muziki wa kizazi kipya (pichani kulia) maeneo ya Kimara, Dar es Salaam. Mpaka nadondosha ishu hii kwenye blog sijajua msala huo uliishia wapi kwakuwa simu ya Jitta ilikuwa haipatikani. Zaidi nitaendelea kucheki naye ili nikufahamishe msala huo uliisha vipi.


Read More......
Posted in | | 0 Comments »