ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU


NATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MBEYA MJINI KUPITIA CHADEMA

NATOA TAMKO RASMI KUHUSU KUHOJIWA KWANGU NA POLISI


Mimi, Joseph Mbilinyi ambaye najulikana zaidi katika anga ya muziki kama “Sugu” ama “Mr II” leo tarehe 29 Juni 2010 natangaza rasmi nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa muda mrefu katika maisha yangu ya kimuziki pamoja na kuimba nyimbo za kuburudisha nimekuwa zaidi mstari wa mbele kuimba nyimbo za kutetea haki za makundi mbalimbali katika jamii na taifa kwa ujumla.

Wakati umefika sasa wa kuhamisha jukwaa la mapambano ya kudai haki kutoka jukwaa la muziki mpaka jukwaa la siasa kwa dhamira ile ile ya kutumia kipaji changu alichonijalia Mwenyezi Mungu kuimba na kuhutubia kwa ajili kuleta mabadiliko ya kweli katika taifa letu.

Nyimbo zangu zimekuwa zikibeba sauti ya watu wasio na sauti ili zisikike na watawala; lakini hata hivyo kwa kipindi chote ambazo nimekuwa nikifanya harakati hizi watunga sheria na wafanya maamuzi ya kisera chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kuongoza vizuri taifa kuweza kufanya mabadiliko ya kweli yenye kuhakikisha watanzania wananufaika na vipaji vyao ambavyo Mwenyezi Mungu amewajalia na taifa linanufaika na rasilimali na maliasili ambazo tumejaliwa kuwa nazo.

Hivyo natangaza nia ya kugombea ubunge ili kuchangia katika kuongeza nguvu ya chama mbadala katika Bunge letu; niwe sehemu ya sauti mbadala katika kutunga sheria, kuwawakilisha wananchi, kuandaa sera na kuiwajibisha serikali kuweza kutekeleza yale ambayo mimi na wanaharakati wenzangu katika sanaa tumekuwa tukiyapigia kelele muda mrefu kupitia muziki wetu na maisha yetu.

Uamuzi wangu wa kugombea ubunge Mbeya Mjini ni haki yangu ya kikatiba na natambua kuwa kwa kuwa mbunge nitafanya kazi ya kuwawakilisha wananchi wenzangu na kama ambavyo wakati wote nimekuwa nikipambana katika harakati mbalimbali ndivyo ambayo nataka niwe mstari wa mbele kupambana katika kuleta maendeleo.

Huu si wakati wa kampeni hivyo niwaahidi wananchi wa Mbeya kwamba nitaeleza mengi kuhusu sera zangu na ahadi zangu kwao mara baada ya kupitishwa na CHADEMA kugombea ubunge katika jimbo letu.

Hivyo, nachukua fursa hii kuwajulisha watanzania wenzangu kwamba siku chache sijazo nitachukua fomu ya chama ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini.

Lakini kwa ujumla uamuzi wangu wa kugombea umesukumwa na harakati zangu za miaka mingi na ufahamu wangu kuhusu hali halisi ya maisha yetu wananchi wa Mbeya Mjini.

Natangaza nia ya kugombea nikiwa ni mgombea mpya kutoka chama mbadala ili kushirikiana na wananchi wenzangu wa Mbeya Mjini kuondokana na siasa za makundi, ukabila, ubaguzi, na migogoro ambazo zimekuwa zikitawala katika Jimbo letu na Mkoa kwa ujumla na hatimaye kusababisha tuwe na uongozi mbovu unaokwamisha maendeleo.

Jiji la Mbeya linakabiliwa na ubovu wa barabara ukiondoa barabara kuu inayokwenda Tunduma; barabara za mitaani ni mbovu wakati ambapo kuna fursa ya kuwa mkoa wenye makaa ya mawe ambayo mabaki yake yangeweza kutumika kukarabati barabara za mitaani Uyole, Soweto na kwingineko.

Natambua kwamba wafanyabiashara wa Mbeya Mjini wanamalalamiko mengi kuhusu kubambikiziwa kodi huku wafanyabiashara wadogowadogo wakiwa wananyanyaswa katika maeneo wanayofanyia biashara kwa kuwa hata mimi mwenyewe nimewahi kuwa mfanyabishara katika soko letu la Mwanjelwa.

Natambua kwamba jiji letu la Mbeya ni kitovu cha elimu katika mkoa wetu hata hivyo lugha zinazotolewa na uongozi wa Mkoa zinawadhalilisha walimu wakati uongozi huo unashindwa kuweka mazingira bora ya elimu na kusababisha Mbeya mjini kuanza kudorora kielimu. Kwa upande mwingine, kadiri mji unavyopunuka ndivyo kero ya usafiri wa wanafunzi inakithiri na shule za pembezoni zinakosa walimu.

Natambua kwamba kwa muda mrefu Mbeya Mjini yetu ina kero ya umeme wakati ambapo tupo jirani na Mgodi wa Kiwira ambao ungeweza kuzalisha umeme wa kututosheleza lakini kutokana na ufisadi tunashindwa kuondokana na hali hii ambayo inasababisha ugumu na kupanda kwa gharama za maisha na kukosa taa za barabarani hali ambayo inaweka mazingira ya kuongezeka kwa uhalifu.

Natambua kwamba viwanda vyetu vya Mbeya Mjini vimeuzwa kwa bei chee na vingine vimeshindwa kuendeshwa na kubaki magovu na kusababisha vijana kukosa ajira na uchumi kuathirika kama ilivyokuwa kwa viwanda vya pamba, mafuta na nyama.

Natangaza nia ya kugombea ubunge wa Mbeya Mjini kwa kuwa naamini kwamba kero ya maji inayotukabili inaweza kuondolewa tukiwa na uongozi mbadala ambao utaweza kutumia vyanzo mbadala vya maji kama mto Mzovwe, Ivumwe na kutoka katika Mlima Igamba.

Natangaza nia ya kugombea Ubunge ili pamoja na kuingia bungeni niweze kuingia katika halmashauri ya Jiji la Mbeya nishirikiane na wananchi wenzangu kuibua ufisadi na udhaifu iliopo unaosababisha ubadhirifu wa fedha za wananchi na mali za umma kama ilivyotokea kwa milioni 68 zilizobaishwa kwenye ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2007/08; tuhuma za kutaka kuuza kiwanja cha wazi eneo la Sokoine na kushindwa kulipa fidia wananchi wa Kata ya Kalobe waliondolewa katika viwanja vyao.

Wakati huo huo; napenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha wananchi wenzangu wa Mbeya Mjini, wapenzi wa muziki wangu, wanachama wenzangu wa CHADEMA na watanzania kwa ujumla kwa jana tarehe 28 Juni 2010 nilikamatwa na polisi kwa kile walichonieleza kuwa kuna malalamiko dhidi yangu kuwa nimemtishia kwa maneno kumuua Ruge Mutahaba kupitia wimbo uitwao “Wanna Kill” uliopo kwenye album iitwayo “Anti Virus”.

Walinikamata saa 5 asubuhi nikiwa naingia ukumbi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya kutoa Mada kuhusu “Tathmini ya Muziki wa Kizazi Kipya na Hatma yake nchini” na kunihoji kwa takrabani masaa matano mpaka saa 10 jioni.

Wameniachia kwa kile walichonieleza kuwa ‘dhamana ya kujidhamini mwenyewe’ na kunitaka niripoti kwao siku ya jumatano tarehe 30 Juni saa 5 asubuhi siku ambayo nilipanga kwenye ratiba zangu kurejea nyumbani Mbeya Mjini kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kabla ya tarehe ya mwisho ya utoaji na upokeaji fomu ndani ya CHADEMA.

Katika mahojiano nao yaliyofanyika Makao Makuu ya Upelelezi Wizara ya Mambo ya Ndani; maofisa usalama (CID) walionihoji walirejea mstari mmoja katika kiitikio cha wimbo husika wenye maneno “I Wanna Kill Right Now” na kusema kwamba mlalamikaji ameutafsiri mstari huo kuwa ni tishio la kutaka kumuua.

Napenda kuwajulisha mashabiki wangu na watanzania wenzangu kwamba nimelieza wazi jeshi la polisi kwamba hakuna wimbo wala maneno niliyowahi kutamka kwa lengo la kukusudia kumuua binadamu yoyote. Niliwaeleza jeshi la polisi kwamba sanaa ya muziki inalugha zake zake za kifasihi.

Maadhui ya wimbo mzima yamejikita katika harakati zangu za siku zote za kupambana na wanyonyaji dhidi ya maslahi ya wasanii Tanzania na wimbo huo una maudhui ya kutaka “Kuondoa ama kuiua dhamira ya mbovu na nia zao ovu”.

Ni vyema mashabaki wangu, wanachama wenzangu na watanzania kwa ujumla wakarejea katika Kamusi mbalimbali za kimataifa ambapoo neno KILL linamaana zaidi ya 10 zikibeba pia maana ya KUKOMESHA, KUONDOA nk.

Katika wimbo huo nimeghani kwa kutumia fasihi mambo ya ukweli yanayotokea katika sekta ya sanaa na wala hauna dhamira yoyote wala maudhui ya kufanya kosa lolote la jinai; hivyo kama kuna mtu ameguswa na ukweli uliomo katika wimbo huo na hakubaliani nao basi aupinge kwa hoja ama akafungue madai badala ya kukimbilia kutaka kuliingiza jeshi la polisi kwenye masuala ya sanaa.

Aidha nimeshangazwa na hatua ya jalada hilo la polisi kufunguliwa ndani ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Wizara ya Mambo ya Ndani yaliyopo Wilaya ya Ilala wakati mimi na mlalamikaji wote ni wakazi wa Wilaya ya Kinondoni.

Baada ya maelezo niliyoyatoa ni matumaini yangu kuwa jeshi la Polisi ambalo lina kazi muhimu zaidi ya kukabiliana na ujambazi na vitendo vingine vya uhalifu ambavyo vinazidi kuongezeka katika Mkoa wa Dar es salaam ambapo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yapo litaelekeza nguvu zake katika kukabiliana na vitendo hivyo vya makosa ya Jinai badala ya kupoteza muda wake kushughulikia masuala ya kifasihi ambayo yanasura ya madai yasiyo na uzito wowote.


Napatikana kupitia: 0716627344 na barua pepe: HYPERLINK "mailto:deiwaka@hotmail.com" \t "_blank" deiwaka@hotmail.com

JOSEPH MBILINYI (SUGU- MR II)


Read More......
Wednesday, June 30, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers & General Enterprises Ltd na mjasiriamali, Bw. Eric Shigongo(pichani), anatarajiwa kuhutubia nchini Marekani katika Mkutano maalum ulioandaliwa na Watanzania waishio nchini humo (Diaspora Council of Tanzanians in America – DICOTA).
Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kwa muda wa siku nne kuanzia Julai 1, mwaka huu katika jiji la Minneapolis, Marriott Hotel, Minnesota, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Aman Abeid Karume, amealikwa kuwa mgeni rasmi. Viongozi wengine watakaohudhuria mkutano huo ni pamoja na maofisa waandamizi na wafanyabishara wakubwa kutoka Serikali ya Tanzania na Marekani.
Aidha, Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Bw. Reginald Abraham Mengi, naye ni miongoni mwa wageni waalikwa wa mkutano huo ambao unafanyika kwa mara ya pili nchini humo ukiwakutanisha Watanzania waishio ughaibuni. Mada mbalimbali zitatolewa na Watanzania waishio ndani na nje ya Marekani.
Katika mkutano huo, Bw. Shigongo anatarajiwa kutoa mada itakayoelezea jinsi ya kufanikiwa kiuchumi katika mazingira ya Tanzania na anatarajiwa kuwahamasisha Watanzania waishio ughaibuni kuwekeza nyumbani Tanzania.
Katika siku za hivi karibuni, Bw. Shigongo amejipatia umaarufu kwa kutoa elimu, ushauri kwa vijana na wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu nchini kupitia mikutano na hafla mbalimbali anazoandaa au kualikwa kwa lengo la kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa kitanzania.
Kwa taarifa zaidi juu ya mkutano huo tafadhali tembelea ukurasa wa Diaspora Council of Tanzanians in America-DICOTA)

Read More......
Friday, June 25, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Diamond akipewa wosia na Youssou Ndour
Pia alikutanana mwanasoka maarufu wa nchini humo, Al Hadji Diouf

Diouf katika pozi

Wiki kadhaa zilizopita mkali wa Bongo Flava, 'Dogo' Nassib Abdul a.k.a Diamond alipewa wosia mzito na mkongwe za muziki wa Kiafrika, Yossou Ndour, akimtaka aongeze nguvu katika game yake ya muziki, kwani mafanikio ya sanaa yake ni zaidi ya kipaji chake kwa hiyo anatakiwa ajitolee sana na asiridhike na sifa ndogondogo ili afike kwenye kiwango cha kimataifa. Diamond aliambiwa hayo pale alipokuwa nchini Senegal kama muwakilishi wa Tanzania kwenye tamasha kubwa la Kampeni ya kutokomeza Maralia duniani lililofanyika katika jiji la Dakar hivi karibuni.

Read More......
Thursday, June 24, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Read More......
Tuesday, June 22, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Read More......
Posted in | | 0 Comments »





Wapenzi wa wakali wawili wa Hip Hop waliyofariki dunia miaka kadhaa iliyopita kwa kupigwa risasi huko Marekani, Hayati Tupac Omar Shakur na Christopher Wallence a.k.a B.I.G wamekumbukwa kwa kutengenezewa sanamu za mastaa hao ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaenzi kwa mchango mkubwa walioutoa kunako game ya muziki huo ambao hivi sasa unatambulika karibu ulimwengu mzima. Hizo juu ndiyo sanamu za mastaa hao waliotingisha ulimwengu.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

"Kaka, pamoja na wa TZ wengi kuwa bize wakati huu wa mambo ya World Cup, ni vyema pia kama wakiwa bize katika kujua na kufuatilia Bunge wakati huu pia kwakuwa ndiyo wakati ambao Bunge limepitisha bajeti ya nchi. Na bila shaka bajeti ndiyo muhimu zaidi kwetu kwakuwa ndiyo muamuziki wa maisha na hatma ya taifa letu masikini.
"Wale wenzetu wanaocheza World Cup wanatambua hilo katika nchi zao na ndiyo maana wamefanikiwa kufika pale na kushiriki mashindano yale, michezo na burudani ni mambo ambayo yana maanisha furaha na starehe katika maisha ya mtu. Na ili mtu afurahi na kustarehe anatakiwa awe ameshapata vitu vyote muhimu na vya msingi katika maisha kama kula kupata elimu, matibabu, kufanya kazi na hata kuvaa na kulala.
"Baada ya kufanikiwa katika vitu hivyo vya msingi ndipo mtu anapoweza kuburudika na kucheza, hivyo ndivyo maisha yalivyo na ndivyo wafanyavyo wenzetu wenye kujielewa. Ni aibu kusikia eti wabunge wetu wanakacha vikao muhimu vya bajeti ya nchi kwa ajili ya kuangalia World Cup", Afande Sele.

Read More......
Sunday, June 20, 2010 Posted in | | 0 Comments »



Hapa wakipiga shoo pamoja

Nas na Marley wakiwa kwenye interview

Katika kile kinachoonesha kwamba Lugha yetu ya Taifa a.k.a Kiswahili inaendelea kupasua anga ulimwenguni, mastaa wawili wa muziki wa Hip Hop Marekani, Nas Escoba na mtoto wa Hayati Bob Marley, Damian Marley wameitupia lugha hiyo kwenye ngoma yao yenye jina la As We Enter. Washkaji hao ambao wamesimama vyema kwenye kolabo hiyo ya ukweli ambayo wameimba kwa kupokezana wametumia maneno ya kiswahili kama “Habari gani”, “Nzuri sana” na kuifanya lugha yetu kutambulika na mataifa mbalimbali duniani. Zaidi icheki ngoma hiyo hapo pembeni huku maneno ya kiswahili yakiwa yamewekewa mishale.



HII NDIYO NGOMA WALIYOTUPIA KISWAHILI


Lyrics: As We Enter

[Damian Marley]
As we enter
Come now we take you on the biggest adventure
[Nas]
Must be dementia, that you ever thought
You could touch our credentials, what's the initials?
[Damian Marley]
You be Jamrock the lyrical official
Send out the order, laws and the rituals

[Nas]
Burn candles, say prayers, paint murals
It is truth we big news, we hood heroes
[Damian Marley]
Break past the anchor, we come to conquer
Man a badman, we no play Willy Wonka
[Nas]
And I got the guns
[Damian Marley]
I got the ganja
[Nas]
And we could blaze it up on your block if you want to
Or haze it up stash box in a Hummer
Or you could run up and get done up
[Damian Marley]
Or get something that you want none of
Unlimited amount you collect from us
Direct from us, street intellectuals

[Nas]
And I'm shrewd about decimals
And my man'll speak Patois
And I can speak rap star
Y'all feel me even if it's in Swahili
Habari Gani

[Damian Marley]
Nzuri Sana
Switch up the language and move to Ghana
[Nas]
Salute and honor, real revolution rhymers
[Damian Marley]
Rhythm piranhas
[Nas]
Like true Obamas, unfold the drama
[Nas]
Word is out, hysteria you heard about
Nas and Jr. Gong gonna turn it out
Body the verse until they scream "murder" out
The kings is back, time to return the crown
Who want it? Tuck your chain, we're due coming
Renegades that'll peel you back like new hundreds
Bet your jewels on it, you don't want to lose on it
Either move on or move on it
[Damian Marley]
Queens to Kingston
Gunshot we use and govern the kingdom
Rise of the Winston, I can see the fear up in your eyes
Realize you can die any instant
[Damian Marley]
And I can hear the sound of a voice
When you must lose your life like mice in the kitchen
[Nas]
Snitching, I can see him pissing on hisself
And he's wetting up his thighs and he trying to resist it
[Damian Marley]
Switching, I can smell him digging up shit like a fly
Come around and be persistent
[Nas]
That's how you end up in a hitlist

[Damian Marley]
Ain't no bad man business
[Nas]
No evidence
[Damian Marley]
Crime scene, fingerprint-less
[Nas]
Flow effortless
[Damian Marley]
Casual like the weekends
[Nas]
No pressure when
[Damian Marley]
We're comfy and decent
[Nas]
We set this off beasting
[Damian Marley]
Hunting season
[Nas]
And, frankly speaking...
Word is out, hysteria you heard about
Nas and Jr. Gong gonna turn it out
Body the verse until they scream "murder" out
The kings is back, time to return the crown
Who want it? Tuck your chain, we're due coming
Renegades that'll peel you back like new hundreds
Bet your jewels on it, you don't want to lose on it
Either move on or move on it
Word is out, hysteria you heard about
Nas and Jr. Gong gonna turn it out
Body the verse until they scream "murder" out
The kings is back, time to return the crown
Who want it? Tuck your chain, we're due coming
Renegades that'll peel you back like new hundreds
Bet your jewels on it, you don't want to lose on it
Either move on or move on it



Read More......
Friday, June 18, 2010 Posted in | | 0 Comments »


Wasanii Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ na Ambwene Yesaya ‘A.Y’ Jumapili wiki hii watatambulisha ‘projekti’ yao mpya ikiwemo ngoma yao ‘Usije mjini’ ndani ya Club Bilicanas. Pia A.Y atatoa shukrani kwa mashabiki wake waliomsapoti na kufanikiwa kupata tuzo kama msanii Bora wa Afrika Mashariki na Kati zilizotolewa nchini Ghana hivi karibuni


Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Prodyuza wa Bakyard, Bratoni akiwa ofisini kwake

"Nimejitolea kurekodi bure nyimbo na vitu vyote vya sanaa kuhusu uchaguzi mkuu wa Oktoba. Nimeanza mwanzoni mwa mwezi huu mpaka Agosti 10, hii ni kwa wasanii wote nchini wenye nyimbo za kuelimisha kuhusu uchaguzi mkuu. Naomba nieleweke vizuri kwamba siyo wimbo au kazi inayohusu chama fulani isipokuwa ni kazi zenye kutoa elimu kwa wapiga kura" - BRATON.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Kwa wale ambao hawajafahamu maana ya neno "KULIPUKA" wacheki na picha hii. Hapa mdogo wangu Robert wa www.burudanikilasiku.blogspot.com ntakuwa nimemkosha ile mbaya, anaweza akaambulia staili hata moja.

Read More......
Sunday, June 13, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Zuhura akiingiza vocal
Mimi pia kuna kitu nilifanya, kikiwa tayari nitawadondoshea wadau

Zurura na prodyuza Villy wa 24/7 Records
Mimi na Villy

Juzikati nilidondoka pande za Mikocheni 'Kwa Warioba' ndani ya studio za 24/7 nikakutana na mwanadada Zuhura a.k.a Limupenzi, tukapiga stori mbili tatu kisha wote tukaingiza vocal. Unajua mimi nilifanya nini?. Endelea kucheki hapa, mzigo ukiwa tayari ntaudondosha kwenu ili tushee idea.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Read More......
Posted in | | 0 Comments »



Kundi la muziki wa asili kutoka Botswana, Matsuwe Tradition Dance maarufu kama Makhirikhiri bado lipo Bongo na kinachofuata hivi sasa ni ziara mkoani Mbeya ambapo litaangusha shoo ndani ya Uwanja wa mpira wa Sokoine Juni 12, mwaka huu kabla ya kumalizia Iringa katika Uwanja wa Samora.
Sisi kama ShowBiz leo tunamcheki kiongozi wa kundi hilo, Moses Malapela ambaye ana a.k.a ya Shumba Ratshega. Wengi hawajui Shumba katoka wapi mpaka kufikia hapa alipo leo kama kiongozi wa kundi la Makhirikhiri mwenye sauti ya kipekee katika ngoma za muziki huo wa asili.
Mchizi alizaliwa 1981 katika kijiji cha Bobonong, nchini Botswana ni miongoni mwa wasanii wa muziki huo waliopitia pilikapilika za hapa na pale. Alianza kama mcheza shoo ndani ya Kundi la Re Tlaa Re Ke Dipitse Cultural Group lililokuwa hapo hapo kijijini kwao.
Baada ya hapo alijimuvuzisha hadi kwenye kundi lingine lililokuwa na jina la Motswedi Cultural Group. Jina la Shumba alilipata kupitia kabila yao, Kalanga likiwa na maana ya Simba huku lile la Ratshega kwa mashabiki wake alipokuwa akipiga shoo.
Alitoa albamu yake ya kwanza kama muimbaji na mchezaji mwaka 2006 ikiwa na jina la Masiela. Albamu hiyo ambayo haikumtambulisha vyema ilifuatiwa na Makhirikhiri 2007 ambayo ilifanya vizuri na kuuzwa katika nchi kibao zikiwemo Botswana yenyewe, Afrika Kusini, Namibia, Zambia na Zimbabwe.
Mwaka huo huo wa 2007, kupitia Tuzo zenye jina la Mascom-Bomu Awards, Makhirikhiri aliibuka na ushindi kama albamu bora ya asili. Mwaka 2008 Shumba aliitambulisha albamu mpya yenye jina la Ntopolela Bichana kupitia wimbo wa Dikhwaere. Mwaka jana wa 2009 akatambulisha albamu nyingine yenye jina la Kukantsu.
Kupitia muziki wake, Shumba ameweza kujiwekea heshima ndani na nje ya nchi yake Botswana, mfano mzuri ni pale alipofanya shoo mbele ya rais wao, Lt General Seretse Khama Ian Khama kwenye sherehe za uhuru na kuwaburudisha mawaziri wote wa nchi hiyo kwenye hafla ya chakula cha usiku.
Akiwa na kundi lake, Makhirikhiri, Shumba amewahi kufanya shoo Afrika Kusini, China, Namibia, Zambia na Angola kabla ya kuja Tanzania. Kutokana na heshima aliyoijengea nchi yake kabla hajaja Tanzania, Rais wao, Lt General Seretse Khama Ian Khama alimkabidhi bendera kwa ajili ya kuitangza zaidi Botswana.

Read More......
Friday, June 11, 2010 Posted in | | 0 Comments »


Jaffarai (kushoto) na Mox

Kutoka pande za Kijitonyama, Dar mchizi aliyewahi kufanya vyema kupitia ngoma yenye jina la ‘Napenda nini’, Jaffari Ally Mshamu a.k.a Jaffarai amesema na ebwanadaah kwamba ‘Demu wangu’, ngoma yake inayofanya vyema hivi sasa tayari imetupiwa kwenye kamera za video na muda wowote inaanza kuuza kunako vituo kadhaa vya televisheni.
Akipiga stori zaidi, Jaffarai alisema kwamba video ya ngoma hiyo imefanyika sehemu kadhaa ndani ya Dar es Salaam chini ya mtayarishaji John Kallage huku ikiwauzisha sura mastaa kibao wa Bongo flava na wadau wa muziki huo ambao ni kipenzi cha msanii huyo.
“Bado naamini kuwa ili msanii afanye kazi nzuri hata kama ni mkongwe lazima aumize kichwa kwa kuandika kazi nzuri, ndiyo maana mimi niko ‘bize’ kuhakikisha kila ngoma ninayotoa inakuwa juu kama hii “Demu wangu’ niliyomshirikisha TID ambaye hakufanya masihara kwenye korasi,” alisema Jaffarai.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Kutoka pande za Rock City kijana SAJNA anayekuja juu kunako game ua miziki wa kizazi kipya amedondoka ndni ya jiji la Dar kwa ishu ya kuitangaza album yake ya kwanza ambayo iko katika hatua za mwisho kukamilika na kwamba inatarajiwa kutelemka sokoni mwezi mmoja ujao.
"Album itakwenda kwa jina la IVETA, itakuwa na jumla ya ngoma kumi zikiwemo IVETA, BINADAMU, MBALAMWEZI, SUBIRA, MGANGA, ROHO MBAYA, NADHIFA na nyinguine. Katika album hii atawashirikisha BELLE 9, LINAH na JOSEFLY, lengo la kuwapa shavu wasanii hao wachache ni kutaka kuonesha kipaji chake zaidi.
Studio zilizohusika kuigonga album hii ni pamoja na TETEMESHA RECORDZ (Kid bwoy), AB RECORDS (Amba), MUSIC LAB (Duke), MZUKA RECORDS (Benja) na A2P RECORDS (Sam Timba)," alisema Kid Bwoy.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


"Inakuweje wana? Ebana nawasukumia mzigo wangu mpya unaitwa 'NAUZA KURA YANGU' ni mkono wa Q. HARAKATI MWANZO MWISHO" Bonta.
Kama bado hujamsoma mchizi huyu kutoka pande za A-Town anawakiliza River Camp Soldier na tayari ngoma huyo imeshaanza kubang kupitia vituo kadhaa vya luninga na televisheni.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Rich One (kulia) akiongea na blog hii kuhusu ujio wao mpya
Baadhi ya wasanii waliodai kujitoa ndani ya kundi la TMK Wanaume Halisi linaloongozwa na Nature, juzi walitangaza kikosi chao kipya kikiwa na jumla ya silaha sita za maangamzi, yaani.
1.RICH ONE
2.MZIMU
3.DAZ P (BWANA MKUBWA)
4.KAKAMAN
5.A-MAN
6.JUMA JAZZ
Jamaa nao wanajiita 'WANAUME' na kwamba siku yoyote kuanzia sasa watadondosha kazi mpya kwa ajili ya kujitambulisha rasmi. ebwanadaah inawatakia safari njema na yenye mafanikio katika game nzima ya mzuki wao.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Aliyekuwa staa wa muziki wa Kiafrika kutoka pande za Gaboni, Oliver N’goma amefariki dunia katika Hospitali ya Omar Bongo iliyopo Libreville huko huko Gabon. Kwa mujibu wa mtandao mwanamuziki huyo aliaga dunia juzi Jumatatu akiwa na umri wa miaka 51.
Olive N'goma a.k.a Noli alizaliwa Machi 23, 1959 pande za Mayumba, Mashariki wa Gaboni akiwa katika familia ya wanamuziki. Ndani ya game ya muziki alikuwa na uwezo mkubwa wa kuandika mashairi, kuimba na kucharaza gita, kazi iliyomfanya akatambulika karibu ulimwengu mzima ilikwenda kwa jina la Bane ambayo aliiachia 1989. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amen.

Read More......
Wednesday, June 9, 2010 Posted in | | 0 Comments »


Shoo ya Temba na Chegge




Michael Ross (Uganda)

Read More......
Tuesday, June 8, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Aliyekua mmiliki wa Bendi ya Chuchu Sound, Yusuf Chuchu a.k.a Mzee Chuchu alifariki dunia huko Nairobi, Kenya Juzi na kuzikwa nyumbani kwao Mwanakweleke, Zanzibar jana Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. AMEN

Read More......
Sunday, June 6, 2010 Posted in | | 0 Comments »

B-12 a.k.a Dazan wa XXL ya Clouds FM ndiye alikuwa stelingi wa shoo nzima

Michael Ross
Wahu
Temba & Chegge
Chegge
Temba
Mwisho wa siku nilikula pozi na Dj Choka
Pia nilishoo lavu na Mtoto wa Mama Said a.k.a Chegge

Juzi ndani ya Club Sun Cirro, Sinza, Dar es Salaam wanangu Temba na Chegge waliangusha 'Vita uwanjani' kupitia shoo ya ukweli iliyopewa jina la Usiku wa Mkono Mmoja. Kama ilivyotarajiwa na wengi, ndani ya uzinduzi huo wa albamu ya kina Chegge ilikuwa ni full shangwe pale mastaa kutoka Uganda na Kenya yaani Michael Ross na Wahu waliposimama stejini na kuonesha uwezo wao. Vijana pia walipewa sapoti ya kutosha na wanao wa TMK Wanaume family bila kulisahau chana la Tip Top Connection.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

A.Y katika pozi
Sean Kingston katika pozi na mwanahabari

"Hali vipi? Napenda kuwashukuru mafans wangu wote walionisupport kwa kunitakia kheri na kunipigia kura katika Tunzo za Ghana zijulikanazo kwa jina la MUSEKE.Kwani nimeshinda East African Song of the Year kupitia wimbo wa LEO.Ushindi huu si wangu peke yangu ni pamoja na Watanzania wote,Mashabiki wa AY na mashabiki wa Muziki kwa ujumla.Nafanya kazi sana,mnanipa support kubwa na Matokeo tunayaona.Mafanikio bado hatujayafiki so MO FAYA. Naenda kampala leo kupiga show katika fainali za Pilsner Djs Spinning.Kutoka kwa A.Y.

KUPIGA SHOO NA SEAN KINGSTON

Pia kama ulikuwa haujafahamu, kuna bonge la ishu limedondoka pande hizi, 'ebwanadaah' likitengeneza kichwa cha habari kisemacho kwamba, A.Y kupiga kolabo na Sean Kingston, ikiwa na maana kwamba siku kadhaa zijazo mchizi atakwea pipa na kwenda kupeperusha bendera ya Bongo katika nchi ya Obama kwa kufanya kazi na staa huyo.

Picha lilianzia ndani ya kituo cha Redio Cloud FM pale Sean Kingston alipokuwa anafanyiwa ‘intavyuu’ kupitia kipindi cha XXL muda mchache baada ya kuwasili Bongo kwaajili ya shughuli nzima ya utoaji tuzo za Kili iliyofanyika hivi kariubuni.

Ndani ya ‘intavyuu’ hiyo ambayo ilirekodiwa kwenye video ya Frank Mtao wa 2Eyez Production, Sean Kingston alisema kwamba msanii wa Bongo anayemkubali zaidi ni A.Y na kwamba alitamani kuangusha naye kolabo, kitu ambacho kiliwafanya wasaidizi wake wawasiliane na Mzee wa Commercio ambaye alipata ‘chansi’ ya kukutana na staa huyo kisha kubadilishana mawazo.

“Nilipokutana na jamaa kweli alisema anavutiwa na kazi zangu, akaniomba tukapige kolabo, ni mtu ambaye hana mapozi na ilikuwa nipige naye ngoma moja hapa Bongo lakini bahati mbaya prodyuza wangu, Hermy Bakawa amesafiri. Kwa kifupi amenipa moyo sana, nikienda huko natarajia kufanya maajabu,” alisema A.Y .

Read More......
Friday, June 4, 2010 Posted in | | 0 Comments »



Hapa jamaa walipoangusha burudani Kanda ya Ziwa
Hapa nikimkaribisha Shumba, kiongozi wa Makhirikhiri aone jinsi ninavyopiga mzigo
Hapa Shumba na wadau wengine wa kundi hilo wakiangalia kazi ninayofanya 'Craphic Desgner'
Hapa nikishoo lavu na mwanadada Linda wa Makhirikhiri
Mdau Cralence 'Mwalumwalu' naye alipata bahati ya kujiachia na mwanadada Selebe
Mdau Walter a.k.a Mcharuko (katikati) ye alikuwa bize na kina Shumba tu
Hapa mimi na Wafanyakazi wenzangu wa Global Publishers tulipata fulsa ya kupiga picha ya pamoja na Makhirikhiri

Siku moja iliyopita mimi pamoja na wafanyakazi wa Kampuni yetu ya Global Publishers tulipata bahati ya kutembelewa na kundi maarufu la muziki wa asili kutoka Botswana, Makhirikhiri linaloongozwa na Moses Malapela a.k.a Sumba Ratshega na kupiga nao stori mbili tatu.
Baada ya kuacha gumzo Kanda ya Ziwa kwa shoo kadhaa za ukweli, jamaa wanatarajia kuacha historia Bongo kwa kupiga kazi ya nguvu ndani ya Ukumbi Diamond Jubilee Ijumaa ya wiki hii kwa kiingilio cha buku 20 kwa VIP na buku 10 kawaida. Mimi pia ntakuwepo kwasababu nawakubali ile mbaya, wewe je?

Read More......
Posted in | | 0 Comments »