ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU



"Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufikisha miaka 26 leo Ijumaa, Julai 30, 2010. Wengi walitamani kufikisha umri kama wangu lakini haikuwa hivyo, so nina kila sababu ya kumshukuru kwa kunipa afya njema hadi hadi hivi sasa. Ninafuraha kubwa ambayo haina kifani, nawashukuru rafiki zangu, mashabiki wangu kupitia sanaa ya filamu na wote walionitakia B'day njema, nawapenda wote". Hayo ni maneno ya Tabia Batamwanya staa wa muvi Bongo ambaye pia aliwahi kushika mataji mbalimbali katika tasnia ya urembo nchini.

Read More......
Friday, July 30, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Mataluma na Temba wakishuka pande hizo
R.O.M.A na Belle 9 pia ndani
Linah, Amini live

Ule mpango wa kujipangusa, yaani ‘Rrraaaaaaaaa’ bado unaendelea na sehemu zinazofuata baada ya Tanga na Zanzibar ni Kanda ya Ziwa, Musoma na Mwanza.
Nalizungumzia Tamasha kubwa la Fiesta 2010 ambalo leo liko pande za Musoma huku timu ya wakali wa Bongo Fleva ikichukua nafasi stejini na kujiopangusa pamoja na maelfu ya mashabiki watakaojitokeza usawa huo.
Primetime Promotion ambao ni waandaaji wa mpango huo wa kujipangusa wamesema na ebwanadaah kwamba upande huo ishu nzima itachukua nafasi ndani ya Musoma Hotel huku wasanii kama Temba, Chegge, Belle 9, Barnaba, Linah, Beatrice William, Amini, Fid Q na wengine kibao wakisababisha kwa kuhakikisha burudani yote inakwenda sawia.
“Baada ya Musoma, kesho Jumamosi itakuwa ni zamu ya Mwanza kwa shoo ambayo itaanzia ndani ya Yatch Club na kufuatiwa na Uwanja wa CCM Kirumba Jumapili, huku msanii Fid Q akiwa ndiyo mwenyeji wetu,” walisema waandaaji.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Mwanadada aliyetengeneza jina kupitia shindano la kufatuta vipaji, Bongo Star Search 2008, Beatrice William, kupitia ebwanadaah amedondosha ushauri wake kwa shindano hilo kwamba hivi sasa wanatakiwa kuangalia mshiriki gani ambaye ana uwezo wa kuandika na kuimba nyimbo zake mwenyewe.
Msanii huyo kutoka pande za Mwanza ambaye hivi sasa anafanya vizuri na ngoma yenye jina la ‘Acha waone’ alifunguka hayo baada ya kuulizwa na safu hii anadhani ni kitu gani kinachowafanya washindi wa BSS washindwe ‘kushaini’ katika game ya muziki.
“Binafsi nadhani umefikia wakati sasa kwa waandaaji na wapiga kura kuangalia nani mwenye uwezo wa kutunga na kuimba, siyo mwenye uwezo wa kuimba nyimbo za watu wengine kama ilivyokuwa kwenye mashindano yaliyopita kitu ambacho kimewafelisha washindi kwakuwa wanashindwa kuandika nyimbo zao,” alisema Beatrice, ambaye kifamilia ni mama wa watoto 3.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Akiwa amepitia milima, mabonde na vikwazo kibao mpaka kufikia mafanikio aliyonayo leo, mwanadada Judithi Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee yuko tayari kusheherekea miaka kumi tangu aingie kwenye game ya muziki wa kizazi kipya kunako miaka ya 2000.
Mwanadada anayo kila sababu ya kusheherekea kwakuwa tangu ajitupie kwenye fani miaka kumi iliyopita, hajawahi kushuka chini au muziki wake kutosikika kwa muda mrefu kupitia vyombo mbalimbali vya habari tofauti na baadhi ya mastaa alioanza nao safari ambao hivi sasa hawajulikani walipo.
Uvumilivu na mishemishe alizogonga mpaka kufikia hatua ya kumili bendi yenye jina la Machozi vinaifanya a.k.a yake, Komando kuwa ya ukweli zaidi kwani ameonesha ni jinsi gani ni jasiri katika kupambana kwa kuipigania sanaa yake mpaka ikampeleka mbali.
Kupitia blog yake Jide amedondosha maneno yanayosomeka hivi. “Tarehe 6 August ni Show Kubwa ya Miaka 10 Ya Lady JayDee….chagueni nyimbo mnazopenda kuzisikia, nitajaribu kugusa kuanzia, Machozi, Binti, Moto, Shukrani na Album ya Combination ya Machozi Band”.
Kama bado haujafahamu ishu hiyo ita-take place pande zipi, mpango mzima utachukua nafasi Mzalendo Pub iliyopo ndani ya mjengo wa Millenium Tower, Makumbusho, Dar es salaam. Ebwana daah! ambayo ni mdau namba moja wa burudani Bongo inaungana na mwanadada Jide katika furaha yake ya kutimiza miaka kumi kwa mafaniko japo bado safari yake kimuziki inaendelea.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Ray C
Mwisho mjengoni BBA All Stars
Mwisho

Mwanadada Rehema Chalamila a.k.a Ray C leo anatokea tena hapa ebwana daah! akiwa na ishu mpya inayomuhusu yeye na ‘X Boyfriend’ wake, Mr. Morogoro a.k.a Mwisho Mwampamba ambaye bado anaendelea kula bata ndani ya mjengo wa Big Brother All Stars huko Sauzi.
Kama bado hujainyaka ishu yenyewe ni kwamba, mwanadada Ray C amefunguka na kumfagilia Mwisho huku akimtakia ushindi mwema katika shindano hilo la BBA kwani bahati kama hiyo huwa haiji mara mbili.
Akipiga stori na Dj Fetty kupitia kipindi cha Bongo Fleva kilichorushwa na kituo cha redio Clouds FM mwishoni mwa wiki iliyopita, Ray C alisema kwamba hakujisikia vibaya Mwisho alipomtaja kama girfriend wake wa zamani kwakuwa anazidi kumtangaza.
“Kwangu iko poa, yeye kunitaja BBA kwakuwa anazidi kunitangaza, ukizingatia kwamba mimi na Mwisho bado tunawasiliana kama marafiki. Kikubwa namtakia ushindi, ajitahidi kwa kuitumia nafasi hiyo aliyoipata mara ya pili vizuri ili arudi Bongo na pesa hizo,” alifunguka Ray C baada ya kuulizwa na Dj Fetty anajisikiaje kutajwa na Mwisho wakati akiingia kwenye mjengo wa BBA?

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Monica katika pozi
...hapa akiwa na shoga yake, Brandy (kulia)

...hapa akijiachia na mbwa wake

Safu yako ya kijanja, Ebwana Dah! Wiki hii inakudondoshea majina ya mastaa wa kiume waliowahi kufanya mapenzi na staa wa R&B pande za US, Monica Arnold. Kwa mujibu wa site ya kiwanja ambayo ipo serious katika kufuatilia uhusiano wa mastaa hasa wa kwa himaya ya Obama, Usher Raymond ndiye anatajwa kuwa mwanaume wa kwanza wa Monica na inaelezwa kuwa walitoka mwaka 1995.
Jarvis Weems anatajwa kuwa wa pili na alichangamka naye kuanzia mwaka 1998 hadi 2003 lakini Monica akiwa kwenye uhusiano huo, mwaka 2000 alimegeka kisela kwa C-Murder.
Young Buck alifaidi penzi la Monica mwaka 2004 na mwaka 2005 akajituliza kwa Rodney Hill.
Jina lake kamili ni Monica Denise Arnold, alizaliwa Oktoba 24, 1980 College Park, Georgia, Marekani. Umri wake ni miaka 29 na ni mhitimu wa High North Clayton High School, Atlanta, Georgia. Safu hii pia inapatikana ndani ya Gazeti la Ijumaa Wikienda linalotoka kila siku ya Jumatatu.

Read More......
Sunday, July 25, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Baadhi ya wasanii na wadau wa burudani watakaodondoka Tanga kesho
R.O.M.A yuko tayari kujipangusa na mashabiki wa pande hizo

Ule mpango wa kujipangusa kupitia tamasha kubwa la Fiesta 2010 utaendelea tena kesho ndani ya Uwanja wa Mkwakwani pande za Tanga kwa shangwe zilezile kama ilivyokuwa Dodoma na sehemu nyingine, huku wasanii kama Mwasiti, Diamond, Kassim, Fid Q, R.O.M.A, Chegge, Temba na wengine kibao wakipiga

Read More......
Friday, July 23, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Katika kuonesha kwamba yuko ‘andastending’ na ile kauli mbiu ya kupambana na gonjwa hatari la Malaria ‘Zinduka’, mwanadada Khadija Shaban a.k.a K-sher alijikuta amejisogeza kwa daktari ili kujua kama kinachomsumbua ni ugonjwa huo au la.
Ishu hiyo ilichukua nafasi pande za Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita wakati mwanadada huyo anayefanya game ya muziki kupitia kundi la Tip Top Connection alipokuwa kwenye ziara ya tamasha la Fiesta inayoendelea hivi sasa hapa nchini.
“Unajua nilikuwana Malaria tangu wiki iliyopita nikapima na kupata dawa, lakini baada ya kufika Dodoma nikawa sijisikii vizuri ikabidi nikapime tena kwenye Hospitali Kuu ya Mkoa nikakutwa na Malaria 3, nikapewa dawa nyingine, hivi sasa nashukuru Mungu naendelea poa,” alisema K-sher.
ShowBiz inampa pole msanii huyo na inamuombea apone haraka ili aendelee kuwakilisha kupitia game ya muziki wake.
Maoni kuhusu K-Sher cheki na sisi kwa anuani zilizopo juu kulia.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Chiller katika muonekano mpya
Ishu mpya kutoka kwa staa wa ngoma ya ‘Tutaonana wabaya’ Aboubakari Shaban Katwila a.k.a Q Chiller iliyodondoka pande hizi wiki hii inasema kwamba hivi sasa mchizi hataki kusikia habari za kushirikishwa (kolabo) katika ngoma za wasanii wengine.
Akipiga stori na blog hii chini ya meneja wake, Khadija Seif wa Dida Fashion UK, Chiller alisema kwamba hivi sasa hataki kusikia habari za kushirikishwa kwasababu yuko tait na ujio wake mpya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu.
“Hivi sasa nipo kwenye mishemishe za kwenda levo nyingine, sihitaji kushirikishwa na msanii yoyote, nimeshawasaidia sana kilichopo mbele yangu muda huu ni kuangalia jinsi ya kuupeleka muziki wangu mbali,” alisema.
Akiwa ametoka chimbo na ngoma yenye jina la Saba mara sabini inayofanya vizuri sasa, jamaa pia yuko tayari kulitaja jina la albamu yake mpya ambayo ni A sing of matureness kwakuwa tayari imeshakamilika kinachofuata ni video za ngoma kadhaa kabla ya kuwapelekea walaji. Kama una maoni kuhusu Chiller cheki na sisi kwa anuani zilizopo juu.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Kava za muvi hiyo
Kanumba mzigoni
'Crazy' Kanumba akimuwakia Hemed

Kutoka kwa staa wa Muvi Indastri Bongo, Steven Kanumba blog hii imepata ishu mpya kwamba mchizi yuko njiani kudondoka na bonge la picha likiwa na jina la Crazy Love. Machache kuhusu mzigo huo msikie Kanumba mwenyewe anavyosema.

"Movie hii hata mimi mwenyewe japo nimecheza lakini naipenda sana na naisubiria kwa hamu,ni moja kati ya movie ngumu nilizowai kucheza na nikamudu sawia,itakuwa mtaani mwezi ujao (wa nane)Movie hii ilinifanya kwa mda wa mwezi mzima kusoma vitabu mbalimbali vya wasomi na watu mashuhuri duniani kama PLATO,KARL MAX,ALEXANDER THE GREAT,SAMUEL TAYLOR nk,Ilinibidi kuwa karibu sana na waalimu wakubwa wa vyuo vikuu ili kujua tabia zao.TAFADHALI SI YA KUKOSA,PATA NAKALA YAKO ORIGINAL,,MOVIE HII IKITOKA NAOMBA MNIAMBIE KWA KUNITUMIA E MAIL MBALI NA MIMI HAPA BONGO NI MSANII GANI WA FILAMU HAPA AMBAYE ANGEWEZA KUCHEZA UHUSIKA HUO?NINA UHAKIKA MAJIBU YATAKUWA HAKUNA....AHAHAHAH SWAHIBA UPO?"

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Mwisho alipokuwa anaingia mjengoni leo
Mr. Morogoro, Mwisho Mwampamba na mrembo Tatiana wa Angola ni miongoni mwa mastaa wa BBA zilizopita waliyopata shavu la kurudi mjengoni leo kuusaka ushindi wa dola laki mbili kupitia shindano hilo ambalo limepewa jina la Big Brother All Star.
Wengine waliyorudi mjengoni ni Jennifer (Mozambique), Kaone (Botswana), Paloma (Zambia), Yacob (Ethiopia), Code (Malawi), Shella (Kenya), Hannington (Uganda), Meryl (Namibia) Uti (Nigeria), Yacob (Ethiopia), Lerato (Afrika Kusini), Sammi B (Ghana) na Munya (zimbabwe).
Ili Bongo iendelee kuwa juu tumsapoti kijana wetu Mr. Morogoro ili aibuke na ushindi kama ilivyokuwa kwa Richard. Jinsi ya kupiga kura na ishu nyingine kuhusu BBA zitakuwa zikidondoshwa kupitia website yao, www.bigbrotherafrica.com.

Read More......
Sunday, July 18, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Akitafakari jambo enzi hizo
Ni furaha kwa kwenda mbele
Walter na Cralence wakiwa ndani ya T-shirt za Madiba
Kwa nyuma zinaonekana hivi
Kwa nyuma kuna ramani ndogo ya Afrika na picha yake

Leo Julai 18, 2010 ni siku ya furaha kwa mzee wetu, Nelson Mandela 'Madiba' a.k.a Baba wa Afrika kwakuwa ametimiza miaka 92 tangu alipokuja duniani. Blog hii inamtakia furaha njema na maisha marefu zaidi ukizingatia kwamba ndiyo kioo cha Afrika kwa sasa. Katika furaha hiyo mi pia nimehusika kwa kutengeneza t-shirt zenye picha kubwa ya Madiba kama unavyoziona. Unaweza kuwasiliana nami kwa anuani zilizopo juu ya blog hii kama unahitaji t-shirt hizo mpya na za kijanja.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu, hatimaye kijana Aboubakari Shaban Katwila a.k.a Q Chiller amerudi tena kwenye game, safari hii akiwa amejipanga kutoka kivingine lengo likiwa ni kupiga ishu kimataifa zaidi. Now ninavyokwambia tayari mchizi keshadondosh ngoma moja kideoni ikiwa na jina la Saba mara sabini ikiutambuliusha ujio wa albamu yake mpya itakayosomeka kama A Sing of Matureness. Kama haujafahamu bado mpango mzima kuhusu Chiller unasimiwa na mwanadada jasiri, Dida kupitia kampuni yake, Dida Fashion UK. Kuna mengi zidi kuhusu ujio wa Chiller, usicheze mbali na blog hii ya kijanja.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Leona akijiachia na mpenzi wake, Lou Al-chamaa

Kuanzia leo kupitia hapa nitakuwa nawadondoshea uhusiano wa mastaa mbalimbali wa kiwanja, yaani nani anajiachia na nani na aliwahi kuwa na uhusiano na nani. Kwa kuanza leo tunacheki na staa wa muziki wa R&B, Leona Lewis. Kama hujafahamu kuhusu maisha yake ya uhusiano, amewahi kutoka na mmoja tu ambaye ameweza kujulikana na kuwekwa wazi.

Lou Al-chamaa ndiye anayetajwa kwamba kuanzia mwaka 2002 mpaka sasa, wamekuwa pamoja na hakuna mwanaume yeyote aliyewahi kuweka chata zaidi ya jamaa huyo.

Hata hivyo, hivi karibuni kuna uvumi ulichukua nafasi kwamba wawili hao wameachana, ingawa hakuna kati yao aliyejitokeza na kuzungumzia taarifa hizo kama zina ukweli au ni longolongo.

Jina lake kamili ni Leona Lewis, umri wake ni miaka 25, urefu wake ni futi 5.7. Alizaliwa Aprili 3, 1985, Islington, London, Uingereza. Ebwana dah! Pia inapatikana ndani ya Gazeti la Ijumaa Wikienda litokalo kila siku ya J’tatu. Hakikisha ulikosi.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Wacha waoneeee!! Betrice

Inawezekana ishu hii ikawa kama ‘sapraiz’ kwa wasomaji wengi wa ShowBiz au mashabiki wa msanii Betrice William ambaye ni zao la BSS 2009 aliyesimama katika game ya muziki wa kizazi kipya hivi sasa akiwa na ngoma yenye jina la ‘Acha waseme’ ikiwa pamoja na video yake.
Kama haujafahamu bado, mbali na kushiriki vyema kunako shindano la BSS na kuonesha uwezo mkubwa katika shoo zake, msanii huyo (picha kubwa katika pozi) ni mama wa watoto wa watatu ambao ni Milee, Abel na mdogo wao Vaines na kwamba yuko taiti na game ili kuhakikisha madogo hao wanapata mahitaji yote ikiwemo elimu.
Akipiga stori na ebwanadaah hii msanii huyo alitamka kwamba, haoni sababu ya kuficha kuwa ana familia kama ilivyo kwa mabinti wengine kwakuwa kwake anajivunia watoto na hata anapoonekana kuwa ‘tait’ na game ya muziki mashabiki wake watambue kwamba majukumu ndiyo yanampa mzuka zaidi wa kazi.
“Huwezi amini, nilijifungua mwanangu wa kwanza nikiwa na umri wa miaka 18, mpaka sasa nina miaka 28, kipindi chote hicho nilikuwa tayari kwenye game ya muziki, japo sikuwahi kutoka kama ilivyo sasa. Wanangu wapo kwa bibi yao (mama yake mzazi) Mwanza pande za Igogo wanaendelea na shule huku mimi na baba yao tukiendelea kuwasapoti kwa kila kitu,” alisema Beatrice.
Kuhusu game msanii huyo ambaye atakuwa mwenyeji wa tamasha la Fiesta 2010 pande za kwao, Kanda ya Ziwa alisema kwamba, baada ya kufanya vizuri na ngoma hiyo, Acha waseme siku kadhaa zijazo atasimamisha jiwe lingine kati ya mawili aliyokwisharekodi. “Zipo ngoma mbili, Dance floo na Ndiyo sababu ambazo nitazikabidhi kwa wadau ili wachague moja ambayo itakwenda hewani, naomba mashabiki wangu waendelee kunipa sapoti ili niongeze mzuka zaidi,”.

Read More......
Friday, July 16, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Wengi wanaweza wakashangaa na kujiuliza inakuwaje? Lakini kwake iko poa tu kwakuwa ni muumini mzuri wa Dini ya Kiislam ndiyo sababu iliyomsukuma kugeukia pande hizo na kufanya kazi ya Mungu mpaka kukamilisha albamu yenye nyimbo nne za Kaswida ikiwa na jina la Mazingira.
Namzungumzia Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Hassan Fella ambaye amesema na ShowBiz kwamba, kila kitu anachofanya na kufanikiwa ni mapenzi ya Mungu ndiyo sababu kubwa iliyomfanya ageukia upande huo kwa kuwasaidia vijana wa Chuo cha Kiislamu chenye jina la Al-Madrasaty Salama kilichopo Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam.
“Mkubwa tumetoa albamu au Nashdi, inaitwa Mazingira ikiwa na Kaswida 4 ambazo ni Ndoa, Ukimwi, Rushwa na Mazingira yenyewe. Pia tumetoa na video yake ikiwa kwenye DVD na VCD kazi zote tunasambaza wenyewe, kwa mara ya kwanza tutazitambulisha Agosti mosi mwaka huu,” alisema Fella.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Mchomvu na B-12 watakuwepooooo!!
Godzilla, Belle 9 ndani
Fiesta siyo burudani peke yake, pia inahusika katika kutoa misaada kwa jamii mbalimbali yenye matatizo kama anavyoonekana Kibonde akiwakilisha misaada kwa kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo pande za Arusha
Kiukweli hii picha ilinivutia ile mbaya. Kushoto ni jirani yangu Henry Mdimu na Chegge, bado sijafahamu walikuwa wanasheherekea Birhday ya nani walipokuwa kwenye ziara ya Fiesta Arusha!..Hebu nambie jamani.

Dodoma mko tayari kujipangusaaa!! Nalizungumzia Tamasha la Fiesta 2010 ambalo lilianza kupagawisha katikati ya wiki iliyopita pande za Morogoro, ikifuatiwa na Arusha na Moshi na sasa ni zamu ya watu wa Dodoma kuondoa matatizo yao kupitia shangwe hizo ambazo zitapigwa kesho ndani ya Uwanja wa Jamhuri.
Primetime Promotion ndiyo waandaaji, ndani ya safu hii wamesema kwamba kama ilivyokuwa sehemu nyingine zilizotangulia ndivyo itakavyokuwa Dodoma kwasababu huwa hawabahatishi na kwamba idadi ya wasanii watakaodondoka pande hizo itakuwa ya kutosha.
Baadhi ya wasanii waliotajwa kushuka Dom ni pamoja na Juma Nature, Fid Q, Keisha, Madee, Kassim, Tundaman, Johmakini, Bele 9, Barnaba, Mwasiti, Linah, Amini, Diamond, Godzilla, Roma, Niki wa Pili, Young Dee, Mataluma na wengine kibao. Baada ya pande hizo msafara utaelekea Tanga kwa shughuli kama hiyo huku timu ya wasanii ikizidi kuongezeka.
Waandaaji hao walisema kwamba, baada ya Tanga, mzigo utatua Zanzibar, kisha Kanda ya Ziwa kabla ya kurudi Dar na kuangusha burudani ya ukweli kwa shoo itakayopigwa kunako sehemu itakayotajwa hivi karibuni.



Read More......
Posted in | | 0 Comments »

MwanaFA akijipangusa na wana wa A-Town jana
TMK pia walionesha uwezo pale Matongee Club, Arusha

Read More......
Sunday, July 11, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Mashabiki wa Moro walivyoitikia wito
Tip Top Connection pia walikuwepo
Hapo nyuma, Jipanguse, Rraaaaaaaaaa!!!

Jipangusee, Rrraaaaaa!! Ndiyo kauli mbiu ya tamasha kubwa la Fiesta 2010 ambalo hufanyika mara moja kila mwaka na kuwakutanisha wasanii kibao kutoka ndani na nje ya Bongo.

Kwa mujibu wa waandaaji, Primetime Promotion, mwaka huu mpango mzima ulianzia pande za Morogoro Julai 7 na kuendelea pale Matongee Club, Arusha Julai 9 ikifuatiwa na Kilimanjaro Julai 10, wilayani Moshi ndani ya Club La Liga.

Baada ya Kilimanjaro shoo itahamia Dodoma, Tanga, kabla ya kurudi Dar es Salaam mwisho wa mwezi huu, kisha Zanzibar, Musoma na sehemu nyingine kibao.

Wasanii kama Mwasiti Almasi ‘Mwasiti’ anayefanya vyema na ngoma yake, ‘Siyo kisa pombe’, Diamond, Madee na wengine kibao ni miongoni mwa vichwa vitakavyosababisha shangwe za ‘Kujipangusa’ katika tamasha hilo la kijanja. Wote sema Rrrrraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Kala na shemeji yetu

Hapa Kala (wa pili kutoka kushoto) akiwa na wana wa pande hizo

Kutoka pande za Uganda a.k.a UG, mwana Hip Hop wa Kibongo, Kala Jeremiah amesema na ebwana daah kwamba zaidi ya miezi miwili sasa yuko nchini humo akipiga madude ya ukweli ikiwa ni njia mojawapo ya kujipanga ili arudi kivingine na pia amefanikiwa kummiliki sista duu wa kona hizo za Museven.

“Niliondoka Bongo zaidi ya miezi miwili iliyopita baada ya kumpata mtu ambaye atasimamia kazi zangu fresh ambaye anaishi huku Uganda, kwa bahati nzuri pia nikafanikiwa kukutana na mrembo huyo ambaye nampenda kupita kiasi tukaanzisha uhusiano. Niliamua kufanya hivi baada ya kuumizwa na mademu wa Kibongo ambao kwangu nawaona kama wazinguaji,” alisema Kala.

Mchizi ambaye kimuziki alijulikana kupitia shindano la kusaka vipaji la BSS mwaka 2007 na kushika nafasi ya nne, alisema kwamba wasichana wengi wa Kibongo hawana mapenzi ya dhati zaidi ya kuweka mkwanja mbele kitu ambacho kinawafanya wasidumu na wanaume.

“Mimi pia nilikuwa nashangaa, hapo Bongo nilikuwa na bahati ya kupata wasichana wazuri lakini sikuwahi kudumu nao, naamini huyu wa huku baadaye anaweza kuwa mke wangu wa milele,” alisema Kala ambaye alikiri kuwa kila akifikiria kurudi nyumbani Tanzania mrembo huyo ambaye hakumtaja jina anahisi kama anamzuia kwa jinsi alivyompenda.


Read More......
Posted in | | 0 Comments »