ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU


Mtoto Sesilia (katikati) akiwa na mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania, Hoyce Temu (kulia) na mlezi wake, Nyarugembe Peter Kambaliko (kushoto)


Ndugu Watanzania,

Jumapili tarehe 11 Septemba, kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa hewani na kituo cha luninga cha Chanel Ten, kilifanya mahojiano na mtoto Sesilia Edward (14) anayesumbuliwa na matatizo ya moyo, ambaye anahitaji kufanyiwa upasuaji wa haraka ili kuokoa maisha yake. Upasuaji huo unatakiwa kufanyika nchini India,

jumla ya dola 15 (sawa na shilingi milioni 24) za kitanzania zinahitajika kuokoa maisha yake. Kama asipofanyiwa upasuaji huo wa haraka atapoteza maisha ndani ya mwezi mmoja.

Baadhi ya Watanzania wameanza kuchangia ili kumsaidia mtoto Sesilia kupitia katika simu za msamaria mwema anaeishi naye huko Mbagala, Bw. Nyarugembe Peter Kambaliko katika nambari zifuatazo:



Tigo Pesa:- 0715 095797

MPESA: – 0762 962467

NMB Account: 2072517079


Hadi sasa zaidi ya shilingi milioni mbili zimeshachangwa, bado michango inaendelea kupokelewa.

Watanzania wenzangu, kutoa ni moyo, usambe si utajiri.


Mtoto huyu ni Mzaliwa wa Kisarawe, yatima na anishi na mlezi aliyemkuta akiwa taabani nyumbani alikokua akiishi na dada anayejishughulisha na shughuli za vibarua vya kulima mashamba ya watu. Alitakiwa kufanya mitihani ya Darasa la Saba na wenzake mwaka huu lakini hali yake haikumruhusu. Ndoto zake ni kuwa mwalimu.


Mlezi wake Peter Nyarugembe, amejaribu kuzunguka katika hospitali mbalimbali bila mafanikio.


Asanteni sana kwa kuokoa maisha ya Sesilia.

Read More......
Thursday, September 15, 2011 Posted in | | 0 Comments »