ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Ukiwa pande za Nanjilikitili halafu unasikia sifa za Bongo Records unaweza kudhani ni studio iliyopo kwenye eneo kubwa kama Kariakoo nzima.
Anayepunguza, basi ataamini ni go-down kubwa halafu ndani yake kuna mitambo ya nguvu, Mkurugenzi Mtendaji wake, Paul Matthysse ‘P. Funk’ analindwa na wapambe 50, ukithubutu kumsogelea umeumia.
Bongo Records ina jina kubwa. Ambao hawajawahi kuiona halafu wanaifikiria kwa ukubwa wa kupitiliza wana sababu ya kuifikiria kwa ukubwa huo.
Imewatoa wakongwe wengi tu, Juma Kassim Kiroboto ‘Nature’, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’, Albert Mangwea ‘Ngwair’ na Jaffari Mshamu ‘Jaffarai’ na wengine wengi.
Mafanikio ya Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Haroun Kahena ‘Inspector’ na Gangwe Mob, Wanaume Family na Halisi na utitiri wa wasanii wengi, kwa namna moja au nyingine, Bongo Records na mkono wa P. Funk ‘Kinywele Kimoja’ vimefanya waking’ara.
Tukumbuke kuwa kipindi kirefu Bongo Records ilibaki kuwa mtawala wa soko la Bongo Flava, ingawa kwa nyakati tofauti kulikuwa na ushindani na MJ Production ya Joachim Kimaryo ‘Master J’ na FM Studio wakati huo Mika Mwamba anasababisha.
Hata hivyo, kinachoonekana hapa ni kuwa P. Funk anashindwa kuiheshimu studio yake wala hajali ukubwa wa jina lake na ndiyo maana anakuwa na migogoro ya hapa pale na wasanii ambao wanakwenda kurekodi.
Ukiachana na vilio vya wasanii chipukizi, hata wakongwe nao imeonekana kasi yao ya kwenda studio hiyo imepungua. Kuna tatizo!
Ipo sifa inayoenea mtaani kwamba P. Funk ni master wa kusimamia vipaji, kwamba wale ambao hawawezi huwa haoni mbaya kuwatoa nishai. Hataki tu kuchukua pesa ya mtu, anaangalia kwanza kazi anayotengeneza. Anahitaji pongezi!
Hilo sawa lakini migogoro na wasanii wake ya nini? Mastaa wengi wanamuogopa kwa sababu dakika mbili mbele anaweza kubadilika na kufanya kitu cha kushangaza.
Ijumaa iliyopita, Mfalme wa Rhymes, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, alipita ofisini kwetu akiwa na furaha. Alikuja kutusabahi na baada ya hapo alitupa taarifa kwamba anakwenda Bongo Records kuchukua kazi yake kwa Majani.
Kwamba walikubaliana aende siku hiyo kazi yake ambayo Afande alirekodi na staa wa Ninao Ninao, Ferouz Mrisho Rehani.
Dakika 10 nyingi, Afande akawa anazungumzia Kituo cha Polisi kwamba amekwenda kumfungulia mashtaka P. Funk kuwa alimtukana, akampiga kofi na kumtishia bastola.
Hilo ni moja la Afande na hatuwezi kuingia ndani zaidi ya kesi hiyo kwa sababu kada za sheria zinazohusika zitafanya uamuzi lakini hapa tunatoa ushauri kiduchu kwa P. Funk.
Aheshimu studio yake kama kweli muziki ni kazi yake. Migogoro na wasanii hatakiwi kuipa nafasi, zaidi studio iwe sehemu ya heshima (ofisi), siyo eneo ambalo wakati wowote linaweza kugeuzwa ringi ya ngumi.
Pamoja na maoni haya, ntajaribu kucheki na Majani ili kujua nini hasa sababu ya kumchapa Afande ili kuweka usawa.

Read More......
Monday, September 27, 2010 Posted in | | 0 Comments »

"Mambo vp kaka? Maoni yangu leo kama mpiga kura, mzalendo na msanii mkubwa ni haya hapa. Viongozi wa dini wasikimbilie kwa MUNGU kuomba amani wakati huu wa uchaguzi bali wanatakiwa wawaambie Tume ya Uchaguzi wasijaribu kuchezea kura za watu kwa kutaka kumbeba mtu au chama chochote mahali ambapo hakikubaliki. Wakifanya hivyo mwaka huu nina hakika amani itavunjika wala maombi kwa MUNGU hayatasaidia na bila shaka itakuwa kama Kenya, kitu ambacho kitafanya viongozi wa Tume ya Uchaguzi na wa Serikali wakutane na mkono wa sheria katika Mahakama ya Kimataifa 'The Heque' chini ya Moreno Ocampo. Siyo kila jambo Wa-TZ tumsingizie MUNGU au shetani wakati tunasababisha wenyewe kwa tamaa za UFISADI wa baadhi ya watu. Tukifanya uchaguzi huru na wa haki daima huwa na amani lakini wizi wa kura, udanganyifu na kuchakachua matokeo ndiyo sababu kubwa ya vita, uasi na matatizo katika taifa lolote"

Read More......
Saturday, September 25, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Kutoka pande za Rock City (Mwanza), mtayarishaji muziki aliyekumbwa na balaa la kuumizwa na mtu asiyejulikana akiwa ndani ya studio yake na kulazwa katika Hospitali ya Bugando, Sandu George Mpanda a.k.a Kid Bwoy amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’.

Akipiga stori na kipindi cha Michano Time kinachorushwa na Kituo cha Radio Passion FM cha Mwanza, chini ya mtangazaji wake Phillbert Kabago katikati ya wiki hii, baba mdogo wa Kid Bwoy, Jose Mpanda alisema kwamba mgonjwa wao amehamishiwa ICU ili kumpa muda mzuri wa kupumzika tofauti na alipokuwa kwenye wodi ya kawaida.

“Napenda kuwatoa wasiwasi ndugu, jamaa na marafiki wa Kid Bwoy kwamba mgonjwa wetu anaendelea vizuri, lakini madaktari wamelazimika kumuhamishia kule kwasababu ya kumpa muda mzuri wa kupumzika. Unajua aliopokuwa amelazwa wodini watu wengi walikuwa wakija kumuona huku wengine wakitumia muda mrefu zaidi kitu ambacho kilikuwa kikimfanya apate muda mchache wa kupumzika,” alisema Jose.

Baba mdogo huyo wa Kid pia alisema kwamba, pamoja na mgonjwa wao kujitambua na kuanza kuongea, wameombwa na dokta anayemshughulikia wasimuulize maswali mengi hasa kuhusiana na tukio zima hadi pale afya yake itakapotengemaa zaidi. Kid alikumbwa na mkasa huo Jumatano ya wiki iliyopita saa 2 usiku akiwa ndani ya studio yake yenye jina la Tetemesha Records. ShowBz inampa pole za kutosha, inaendelea kumuombea apone haraka ili arudi katika hali yake na kulisukuma gurudumu la muziki wa Bongo Flava.


Read More......
Friday, September 24, 2010 Posted in | | 0 Comments »







Kutoka ndani ya kiwanda cha muvi Bongo, wiki hii Mpaka Home imedondoka na kipaji kinachokuj kasi kunako mradi huo, namzungumzia mwanadada Monica Malaki aliyeuza kupitia filamu ya Hot Friday.

Mengi kuhusu yeye na maisha yake kwa ujumla chungulia intavyuu ya kijanja hapo chini.


Mpaka Home: Sema Monica, historia yako kwa ufupi ikoje?

Monica: Nilizaliwa mwaka 1988 Moshi, Kilimanjaro, nampenda mama yangu mzazi kuliko vitu vyote.

Mpaka Home: Vipi kuhusu suala zima la elimu?

Monica: Niliishia kidato cha nne tu baada ya kupata elimu ya msingi hapa hapa Dar es Salaam.

Mpaka Home: Lini uliingia katika tasnia ya muvi Bongo?

Monica: Niliingia mwaka 2004, ila niliibuka zaidi 2008 kupitia filamu ya ‘Hot Friday’ kwani nilipigiwa simu kibao za pongezi kwa kazi nzuri.

Mpaka Home: Nani aliyegundua kipaji chako?

Monica: Vicent Kigosi ‘Ray’, binafsi namshukuru sana maana ndiye aliniita na kunieleza kwamba nina kipaji cha kuigiza.

Mpaka Home:Kwa sasa mashabiki wako wategemee nini kutoka kwako?

Monica: Kuna filamu kibao ambazo nimecheza na wakali mbalimbali ambazo zinakuja kuwakimbiza.

Mpaka Home: Unaweza hata kuzitaja chache?

Monica: Hapana,siwezi kwa sasa..ila wakati muafaka ukifika nitazitaja.

Mpaka Home: Nje ya kuigiza unafanya nini?

Monica: Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) ambapo nachukua Stashahada ya Masoko nikiwa mwaka wa pili.

Mpaka Home: Unautumiaje muda wako huku katika kuigiza filamu na wakati huo huo unasoma?

Monica: Napenda sana kusoma na napenda sana kuigiza, hivyo muda wa kusoma ni wa kusoma na muda wa filamu ni wa filamu.

Mpaka Home: Lakini ni vigumu kuwatumikia mabwana wawili?

Monica: Ndio maana nimekuambia kwamba kila kitu na muda wake, sio kwa wakati mmoja.

Mpaka Home: Vipi una mpenzi?

Monica: Nikose mpenzi tena…miye !

Mapaka Home: Kwanini usikose mwaya?

Monica: Ninatatizo gani? Kwa kifupi ninaye ila hayuko hapa nchini kwa hivi sasa.

Mpaka Home: Yuko wapi na anaitwa nani?

Monica: Yuko nchini Italia kibiashara, nisingependa kumtaja kwa jina kwa sasa, mpaka baadaye kidogo.

Mpaka Home: Nije lini kuchukua jina lake?

Monica: (Anacheka) Aaaah! Bado muda ukifika hata mimi mwenyewe nitakutafuta ili nikutajie.

Mpaka Home: Ulishawahi kuachwa?

Monica: Sijawahi ila mimi n’shawatosa wengi wenye mapenzi ya kuigiza.

Mpaka Home: Unamaanisha nini unaposema mapenzi ya kuigiza?

Monica: Aaah bwana wee nani anataka mapenzi ya kudanganyana? Mimi nikiona mtu simuelewi elewi namtosa tu.

Mpaka Home: Vipi, jamaa ndio yuko kiwanja huku nyuma mapedeshee hawakusumbui kukutaka kimapenzi?

Monica: Mimi ni mtoto wa kike, nakwambia wapo hata vigogo ambao wananitokea lakini najitambua pamoja na kuwepo kwa vishawishi kibao lakini napenda kutumia msemo wasasa ‘SIDANGANYIKI’.

Mpaka Home: Unaweza kumwanika hadharani hata kigogo mmoja anayekufukuzia ili liwe fundisho kwa wengine?

Mpaka Home: Unajua kupika?

Monica: Utakimbia…. Unaweza kujing’ata vidole

Mpaka Home: Wazazi wako ni wapande za wapi?

Monica: Wanaishi Mbezi ila asili yetu ni Kilimanjaro

Mpaka Home: Wasanii wengi wa kibongo hasa chipukizi huteswa na rushwa ya ngono pale wanapotaka kupewa nafasi ya kuigiza, vipi wewe ulishawahi kupatwa na mkasa kama huu?

Monica: Ni kweli lakini kwa bahati mbaya sijawahi kukumbwa na mkasa huu.

Mpaka Home: Unasemaje kuhusu tasnia ya filamu hapa Bongo?

Monica: Ni ngumu, kikubwa ni kukaza msuli ili kuweza kuliteka soko la filamu.

Mpaka Home:Tunashukuru sana Monica kwa ushirikiano wako

Monica: Asanteni sana, karibuni tena.

Read More......
Wednesday, September 22, 2010 Posted in | | 0 Comments »

"Mkubwa za leo. Baada ya kutoa ngom ya KR, 'Choo cha kike' na TMK Family kutoka na kazi yenye jina la 'Wapinzani' ikimshirikisha Q Chiller, Mkubwa nimetengeneza ngoma yenye jina la Tatu 1 kwa ajili ya kuwahimiza vijana wenzangu kujitokeza siku ya kupiga kura. Imerekodiwa katika chumba cha studio za Poteza Rec iliyoko TMK, nimemshirikisha producer wangu anaitwa Suresh. Ngoma itatoka wiki hii,"

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Mlela
Hemed

Baadhi ya wadau wa sanaa ya muvi bongo waliyoguswa na bifu la wasanii wawili, Yusuf Mlela na Hemd wamedondosha maoni yao wakiwashauri vijana hao ambao wamekuwa wakilumbana kupitia baadhi ya vyombo vya habari, huku wakitishia kuchapana makonde. Zaidi kuhusu maoni hayo cheki hapo chini.

Kadole wa Dar : Mimi nadhani anachokifanya Hemed ni kama ushamba , katika hali ya kawaida huwezi kujisifu mbele ya chombo cha habari kuwa umempiga fulani ngumi. Kwa hili nahisi hakuwa sawa.
Baba Calvin wa Kinondoni Dar : Hawa vijana walitakiwa kutumia busara zaidi kuamua suala lao kwani walinavyokashifiana kupitia vyombo vya habari wafahamu kwamba hata soko la filamu zao wanalichafua. Kama wanaweza bora wawe na wasemaji wao wenye uwezo wa kuchambua jambo la kuongea, ni aibu kwa tukio kama hilo, nathubutu kusema hakuna staa wala supa staa kati yao.
Saida wa Mwanza: Mimi nalipongeza gazeti la Ijumaa kupitia hapa ShowBiz kwa kuliona hilo. Ushauri wangu kwao nawataka kwanza watambue umuhimu wao kwenye jamii, pia watambue kuwa wanatazamwa na watu wengi, wakubwa kwa watoto, hivyo waache bifu zisizokuwa na maana.
Kulwa wa Temeke, Dar: Mlela na Hemed wote siyo mastaa, kati yenu hakuna anayemfikia Kanumba wala Ray. Badala ya kufanya kazi ili mzidi kupaa kisanii mnaanza kutuletea bifu zenu za ajabu, nyie bado ni chipukizi sana fanyeni kazi acheni hizo.
Mussa wa Kilwa Masoko: Hemed unajifanya unajulikana Afrika nzima kwa kipi? Acheni majigambo, nyie bado mna safari ndefu kwenye sanaa hamuwezi kuwafunika wakongwe kwa staili hiyo.
Kalunde wa ILALA, Dar: Nadhani hao jamaa hawajijui kama ni kioo cha jamii, nawashauri waende kwa madaktari kucheki vichwa vyao, kwa maana hadhi waliyonayo kama ni wazima kweli hawawezi kufanya ishu kama hizo za kurushiana maneno machafu kwenye vyombo vya habari.
Mama Idd wa Kigamboni, Dar: Nyie vijana wote ni kioo cha jamii, tumieni busara badala ya kuanza kutukanana ovyo. Hivi mnadhani watoto watajifunza nini kutoka kwenu? Acheni hizo.
Light wa Moro: Namshauri Mlela aachane na bifu kwani anashusha heshima yake katika jamii kwakuwa yuko juu na anajitahidi katika sanaa.
Manyama wa Musoma: Hao wote hakuna staa kati yao kwani tumeshajua hiyo ni janja yao tu ya kujitafutia umaarufu, zaidi wanataka kutujaribu akili zetu.
Paparazi Venance wa Dar: Kama mnafikiri kazi ya sanaa inaboreshwa kwa kuwa na bifu basi Kibongobongo mnajiharibia, hakuna jipya mnalolileta kwetu zaidi ya kutuzingua. Fanyeni kazi, acheni bifu zenu zisizo na malipo, hii Bongo msitake kujifananaisha na akina Kanye na 50 Cent nyie bado andagraundi.
Kumbukeni ya Mr. Nice na Dudubaya walivyojimaliza kwa ugomvi wao.

Read More......
Friday, September 17, 2010 Posted in | | 0 Comments »




Kama nilivyowadokeza mwanzoni mwa wiki hii kwamba, leo Ijumaa kupitia kwenye safu ya ShoBiz iliyopo ndani ya Gazeti la Ijumaa ntadondoka na ishu kuhusu ujio mpya wa kundi la Hotpot Family. Kwa wale wa wapenzi wa ebwanadaah mnaipata kupitia hapa.
Baada ya kupotea kwenye game ya muziki wa kizazi kipya kwa takribani miaka kadhaa, familia iliyowahi kufanya vyema katika tasnia hiyo, Hotpot Family imerudi upya ikiwa na sura tofauti huku waasisi wake wakiwa na maneno kadhaa ya kuongea.
Akipiga stori na ebwanadaah kiongozi wa familia hiyo, Anselem Typhone Ngaiza ‘Soggy Dog’ alisema kwamba walichokifanya hivi sasa ni kuirudisha familia ikiwa katika muonekano mpya ili kuwapa nafasi chipukizi wanaoibuka waweze kuonekana.
“Unajua siku hizi chipukizi wanapewa nafasi kubwa kuliko sisi wakongwe, ndiyo maana tunakuwa kimya, siyo kwamba sina kazi, nina ngoma kibao ndani lakini sizitoi kwa sababu hiyo, sijajua ni kwanini wadau wanafanya hivyo. Ndiyo maana tumeamua kutoka na vijana.
“Mimi na Suma G kama wakongwe japo hatupewi heshima hiyo tumewapa nafasi kubwa wasanii wanaotoka kupitia Hotpot Family kwenye ngoma tuliyoiachia hivi karibuni ikiwa na jina la Wanamipango iliyofanyika Makavell Records,” alisema.
Kwa upende wake Suma G alisema na blogu hii kwamba, Hotpot Family ilikuwa inajipanga na sasa ndiyo kipindi chao cha ‘kushaini’ kwakuwa wamerudi tofauti huku wakiwa na nguvu mpya kutoka kwa vichwa kama Another One, Young Page, Baby Baby, Chorus B, na Blast Salim.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Hatumwi mtoto dukani Mbeya, wana wa Uyole, Mafiati,Mwakibete, Mwanjelwa, Isanga, Nzovwe, Soko Matola, Ghana, Majengo na mitaa mingine ya jiji hilo, macho na fikra zao ni sehemu moja tu usiku wa leo. Ni ndani ya Ukumbi wa Mtenda Sunset.
Kunani? Jibu ni kwamba Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, leo anaweka kando gwanda na kuvaa jeans na baada ya hapo atasomeka katika shoo kali ya Hip Hop lakini atasindikizwa na wana wengine wa muziki wa kizazi kipya.
Sugu a.k.a Mr. II, atapiga mzigo mkali kuthibitisha ukongwe wake wa zaidi ya miaka 20 kwenye MIC, atasimama jukwaani zaidi ya saa nzima akikamua shoo ya kweli ya Hip Hop, lakini watakaoingia ukumbini pia wataburudika na Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, Ferouz Mrisho Rehani, Abbas Hamis Kinzasa ’20 Percent’, Danny Msimamo, Fred Maliki ‘Mkoloni’, Gerald Mwanjoka ‘G Solo’, Mapacha ‘Maujanja’ na Isanga Family’.
Akifafanua kuhusu kupanda jukwaani na kuvua kombati ya CHADEMA, Sugu alisema nasi kuwa anafanya hivyo leo, ikiwa ni onesho maalum la kukusanya michango ya kampeni.
“Leo gwanda pembeni, navaa jeans na kushika MIC. Jukwaa moja na Afande, Ferouz, Mkoloni, 20 Percent, Msimamo, Isanga Family na wengine. Ni shoo maalum ya kuchangia kampeni. Tumegawa kadi maalum ambapo kuna maeneo zinanunuliwa kama njugu. Kila kadi tunauza shilingi 10,000.”

Read More......
Thursday, September 16, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Hatimaye kundi la Hotpot Family limeibuka tena likiwa na sura mpya. Je, nini wamerudi nacho na malengo yao kunako game hii? Bila kusahau majina ya memba wapya na kauli ya kiongozi wao, Soggy Dog usikose kucheki ShowBiz ya Gazeti la Ijumaa litakalotoka Ijumaa ya wiki hii.

Read More......
Tuesday, September 14, 2010 Posted in | | 0 Comments »


Enzi zile wakati tukiwa bado wadogo tulikuwa tukiheshimu sana sehemu za makaburi, wala hatukuruhusiwa kucheza maeneo hayo kitu ambacho kiendelea kutujenga baadhi ya watu na kuziheshimu sehemu hizo muhimu hadi hii leo. Lakini siku hizi makaburi yamekuwa yakionekana kama kitu cha kawaida kwa baadhi ya watu kama anavyoonekana jamaa huyu ambaye aliamua kuuchapa usingizi juu ya kaburi wakati waombolezaji wenzake wakiendelea na shughuli ya mazishi ya marehemu Perfect Kagisa 'P. Diddy' yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Dunia yamkumbuka, bado ni shujaa wa mauzo katika Hip Hop


Afen Shakur, mama mzazi wa Tupac
Pac, Snoop (katikati) na Suge Knight
Picha hii ilipigwa dk 20 kabla hajauawa
Tarehe kama leo mwaka 1996, mchawi wa mauzo katika Hip Hop duniani, Tupac Amaru Shakur alifariki dunia baada ya kuishi duniani miaka 25 tu.
Alifariki dunia baada ya kutawala ‘game’ kwa miaka 6 mfululizo lakini kazi yake imeendelea kumuweka chati ya juu mpaka leo. Wachambuzi wengi wanapendekeza Tupac a.k.a Makavelli The Don kuwa Mfalme wa Hip Hop Duniani wa muda wote.
Tupac anapewa cheo hicho kwa kutazama vitu vingi, tungo zake zilivyobamba, mapinduzi makubwa aliyoyafanya katika Hip Hop, jinsi alivyoweza kubadili vijana wengi Marekani ambao waliishi kwa itikadi zake lakini yote kwa yote, Tupac a.k.a King Killuminat anasimama kuwa mtetezi wa haki za binadamu.
Alikuwa na kipaji kikubwa, aliweza kurap kila kitu alichohitaji, alipoamua kuimba jiwe aliandika mashairi yanayojitosheleza na kukuvutia usikilize. Staili yake ngumu imebaki kumuweka wa kipekee, kwani wengi wamejitahidi kumuiga wameshindwa.
Uwezo wake wa kuandika mashairi siyo tu ulitokana na kipaji, bali pia ulinolewa na shule. King Makaveli baada ya kumaliza Paul Laurence Dunbar High School, alipelekwa na mama yake kwenda kusomea sanaa Baltimore School for the Arts ambako alijifunza kuigiza, kuandika mashairi, staili ya Jazi na kucheza kwa kuigiza bila kutoa sauti (ballet).
Alivyorap kiitikio cha Hit em Up imebaki mtihani hata kwa mastaa wakubwa wa Hip Hip wa sasa, wengi wamejaribu wameshindwa lakini inaaminika Eminem peke yake ndiye anayeweza.
Alikuwa mwana Hip Hop aliyefungua njia kwa wengine kwa kukamata namba moja mfululizo kila alipotoa rekodi zake. Gazeti la Blender lilifanya tathmini na kumtaja Tupac kwamba ndiye mtu anayeheshimiwa zaidi kwenye muziki duniani (Most Overrated Person in Music).
Maajabu yake makubwa ni kwamba aliuza nakala nyingi baada ya kufa kuliko akiwa hai, hii imetokana na hazina ya mamia ya nyimbo alizoacha amerekodi studio lakini akafa kabla hajaziachia.
Ameuza zaidi ya nakala milioni 75 duniani na hiyo imemuweka kwenye kundi la wanamuziki bora kwa mauzo duniani. Katika Hip Hop anashikilia nafasi ya pili nyuma ya Eminem, lakini Pac anapewa heshima kwa sababu alifanya muziki kwa muda mfupi mno.
Akina Jigga, P Diddy na wengineo licha ya kuishi muda mrefu kwenye muziki lakini hawajaingia kwenye rekodi ya kuuza. Walikuwepo wakati Pac akitawala soko la Hip Hop enzi za uhai wake na ameendelea kuwapiga bakora sokoni akiwa kaburini.
Sifa kuu ya Tupac ni kwamba hajawahi kuharibu sokoni, albamu zote akiwa hai ziliuza Gold na Platinum. Ni albamu moja tu ya mwaka 2006, iliyotoka miaka 10 baada ya kifo chake “Pac’s Life” ndiyo haikufikia hadhi ya Gold lakini zilizotangulia alifumua Multi-Platinum za kutisha.
“Alistahili kila alichopata. Umaarufu na fedha. Alikuwa milionea akiwa kijana mdogo (miaka 19), alistahili kwa sababu kichwa chake ni madini,” hii ni comment iliyotolewa na mdau wa muziki kusindikiza kifo cha mwanamuziki huyo.
Kuna wanaoamini kuwa mapinduzi ya Tupac kwa kumtetea mtu mweusi Marekani hasa kupitia albamu yake ya kwanza ya mwaka 1991 (2Pacalypse Now) yana maana kubwa kuliko hata maajabu ya Barack Obama kuchaguliwa kuwa Rais wa taifa hilo kubwa duniani.
Kwamba Tupac alibadili fikra za watu, akawapandisha watu mizuka na kuishi kwa itikadi zake.

SAFARI YA KIFO:
Septemba 7, 1996, Tupac alihudhuria onesho la ndondi la Mike Tyson na Bruce Seldon kwenye Ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas. Picha za mwisho zinamuonesha akikumbatiana na Tyson baada ya pambano. Baadaye wakiwa MGM, mpambe wa prodyuza wa Pac, Suge Night alimwambia Pac kwamba Orlando Anderson ‘Baby Lane’ alikuwepo ukumbini hapo.
Pac alimshambulia Anderson ambaye alikuwa memba wa Kundi la Southside Crips kwa kushirikiana na Suge pamoja na wapambe wao. Walipotoka hapo walielekea Klabu ya Death Row inayoitwa 662 na alikuwa anaendeshwa na Suge kwenye gari aina ya BMW 75il sedan 1996 (toleo jipya kwa wakati huo). Walikuwemo pia wapambe kibao.
Saa 4:55 usiku gari likiwa limesimama kwenye taa nyekundu za barabarani, Tupac alishusha kioo akapigwa picha na ‘kameramani’ aliyemwomba. Kati ya saa 5:00–5:05 usiku, walikamatwa Las Vegas Blvd na polisi wa pikipiki kwa kuendesha gari wakiwa wameweka sauti kubwa na kutokuwa na leseni ambayo baadaye ilipatikana, hivyo wakaachiwa bila faini yoyote.
Saa 5:10 usiku walisimama kwenye taa nyekundu kwenye Barabara ya Flamingo, Tupac alisimama kupitia rufu ya gari na kuzungumza na warembo wawili kwenye gari nyingine, akawaalika Klabu 662. Saa 5:15 usiku gari toleo la zamani aina ya Cadillac ambalo lilikuwa na namba isiyojulikana, lilishusha kioo usawa wa Tupac na kumshambulia kwa risasi kifuani.
Moja ya risasi ilipiga kwenye pafu la kulia la Pac. Alipelekwa Hospitali ya University Medical Center ambako alifariki siku sita baadaye (Septemba 13) baada ya upasuaji wa kubadilisha pafu lililoharibika kufeli. Miezi sita baadaye, yaani Machi 1997, Biggie naye aliuawa kwa risasi, shambulio ambalo linadaiwa kufanywa na watu wa Pac.

MAJIVU YAKE YAVUTIWA BANGI
Tupac alianzisha Kundi la Outlawz Immortalz mwaka 1995 ambalo alilitumia kwenye matamasha yake pamoja na kulishirikisha katika kibao cha kihistoria, Hit em Up.
Mwili wake ulizikwa kwa kuchomwa. Kituko ni kwamba memba wa Outlwaz walichukua sehemu ya majivu yake na kuyachanganya na bangi ambazo walivuta kama kumpa heshima.

Read More......
Monday, September 13, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Genevieve katika pozi

Miss TZ 2010, Genevieve Emmanuel Mpangala (katikati) akiwa na mshindi wa pili, Glory Mwanga (kushoto) na mshindi wa tatu, Consolata Lukosi mara baada ya kutangazwa washindi juzi kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam

Read More......
Sunday, September 12, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Z-Anto n Madee baada ya shoo
Kijana aliyepata kufanya vyema kunako game ya muziki wa kizazi kipya, Z-Anto juzi kati alionesha dalili za kurudi ndani ya kundi lililomtoa, Tip Top Connection baada ya kudandia stejini na kusapoti uzinduzi wa kundi hilo uliyopigwa ndani ya Club Sun Nsirro iliyopo pande za Sinza, Dar.
Ilikuwa kama 'sapraizi' wakati MC wa shughuli hiyo, Mwalubadu alipomtaja Z-Anto kuwa anapanda stejini na kusapoti uzinduzi huo, wengi hawakuamini kwakuwa 'dogo' aliondoka kundini kwa jazaba huku akianika madai yake kwa viongozi wa Tip Top kunako vyombo kadhaa vya habari.
Alipopanda jukwaani aliwakumbusha mashabiki wake kwa ngoma ya Binti kiziwi kabla ya kumalizia na hii inayotamba hivi sasa ikiwa na jina la 'Kisima cha malovedavi'. Baada ya tukio hilo ebwanadaah ilimtafuta memba wa kundi hilo, Madee na kumuuliza inakuwaje mchizi karudi kundini kimya kimya? "Anto bado hajarudi kundini, lakini tupo katika maongezi, inawezekana tukawa naye tena pamoja," alijibu.

Wengine waliokuwepo kwenye uzinduzi huo na kutoa sapoti ya kutosha ni hawa hapa chini.


Kabla ya kupanda steji Linah aliweka tumbo fresh


Mwasiti naye alifanya vivyo hivyo ili kuongeza nguvu

Dj Choka na Lulu pia walikuwepo
Kassim baada ya shoo
Young Dee alisapoti
Mfalme wa Sala Sala, Goldzilla alionesha kiwango
Mimi pia (wa pilia kushoto) niliwakilisha na wana. Thanks Dj Choka kutugonga picha hii

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

IKIWA KATIKA MUONEKANO MPYA BAADA YA KUBORESHWA BLOG YAKO YA KIJANJA, ebwanadaah INAWATAKIA WAISLAMU NCHINI KOTE SIKUKUU NJEMA YA EID NA KUWAOMBA WASHEHEREKEE KWA AMANI NA UTULIVU KAMA ILIVYO DESTURI YETU.

EID MUBARAK, MUENDELEE KUWA PAMOJA NA ebwanadaa KWA ISHU ZA UKWELI.

Read More......
Friday, September 10, 2010 Posted in | | 0 Comments »


Hatimaye ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu imewadia. Vijana kutoka pande za Manzese, Dar, Tip Top Connection leo Siku Kuu ya Eid watamaliza kazi iliyokuwa mbele yao kwa utambulisho wa albamu mpya, Bado Tunapanda utakaopigwa ndani ya Club Sunsiro iliyopo pande za Sinza. Unaonaje baadaye baadaye tukajiachie na wana? Siyo ishu ya kukosa.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Kutokana na ushindani uliyopo kunako sanaa mbalimbali ikiwemo game ya muziki wa Bongo Fleva unawafanya wasanii wengi kuwa wabunifu ili kuwavutia mashabiki wao, kitu ambacho kimewafanya baadhi yao kufanikiwa.
Kala Jeremiah ni miongoni mwa mastaa wa Bongo Fleva ambaye ameibuka na kali ya mwaka kwa kuvaa viatu vyenye rangi mbili tofauti (chekundu na cheusi) ikiwa ni staili yake mpya ya uvaaji baada ya kupotelea Uganda kwa kipindi fulani kabla ya kurudi Bongo na ngoma kadhaa.
“Kaka nimeamua kuja kivingine kama walivyokuwa Kriss Kross, siunajua tena mambo ya ubunifu, lazima kwenye game uwe mjanja,” alisema Kala ambaye wiki iliyopita ameachia ngoma yake mpya yenye jina la Miss Uganda itakayofuatiwa na video yake ambayo pia imepigwa pande hizo za UG.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

P Diddy enza ya uhai wake
Maimartha (katikati) akiwa kwenye huzuni baada ya kupata taarifa za msiba

Aliyekuwa mpenzi wa mtangazaji wa kituo cha tlevisheni cha TBC 1, Maimartha Jesse, Perfect Kagisa 'P Diddy' amefariki dunia ghafla leo mchana alipokuwa kwenye mizunguko yake katikati ya jiji la Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Zaidi kuhusu msiba huu mzito usikose kuchungulia Gazeti la Ijumaa siku ya Ijumaa na endelea kucheki hapa ebwanadaah.
Mungu alitoa, Mungu ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Read More......
Wednesday, September 8, 2010 Posted in | | 0 Comments »